1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana wanaume watahiriwa kwa ajili ya kinga

5 Mei 2017

Watu millioni 20 katika bara la Afrika wanatarajiwa kutahiriwa. Kuna baadhi ya jamii wanaamini kuwa kutahiriwa huku kwa wanaume ni hatua moja ya kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi.

https://p.dw.com/p/2cUy2

 

Berlin Pressekonferenz Beschneidung in Afrika
Prince Hillary Mabola akiwa Berlin katika mkutano na waandishi wa habariPicha: DW/D.Pelz

Lakini swala hili limezua mjadala na wanaharakati wanapigana kuiondolea mbali hatua hii ya kutahiriwa kwa ajila ya kujikinga na ugonjwa wa ukimwi.

Mwanaharakati kutoka Kenya Prince Hillary Maloba anasema anajua hasa maumivu ya kutahiriwa na ni kitu ambacho hawezi kusahau. Maloba alitahiriwa alipokuwa mtoto, huu ndio utamaduni wa kabila yake. Maloba anaona suala la  mashirika kutoka nje kwa miaka kadhaa sasa yanaowatahiri wanaume barani Afrika  kwa ajili ya kinga ya ukimwi, kuwa ni kama kashfa.

"Inawezekana vipi? Kabila langu, wamekuwa wakiwatahiri watoto wao, wanaume zao, waislamu pia wamekuwa  wakitahiri watoto wao na bado wanapata ukimwi na kufa," alisema Maloba siku ya alhamisi alipokuwa mjini Berlin.

Berlin Pressekonferenz Beschneidung in Afrika
Mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin juu ya kutahiriwa.Picha: DW/D.Pelz

Prince Hillary Maloba ni mwanaharakati mwenye mradi unaoiotwa VMMC Experience Project ambao unapinga kutahiriwa kwa wanaume kwa ajili ya kinga ya ukimwi. Muungano wa mashirika ya Ujerumani wanaunga mkono mradi wake huu. Na pia wanaunga mkono " siku ya kimataifa ya uamuzi binafsi juu ya kutahiriwa" itakayofanyika May 7. Siku hii inatarajiwa kuadhimishwa ili kuzuia suala la kutahiriwa kwa ajili ya kinga kwa ugojwa wa ukimwi barani Afrika kote.

Lakini shirika la afya duniani pamoja na mpango wa umoja wa mataifa wa ugojwa wa ukimwi wana mtazamo tofauti. Mashirika hayo yameandika katika mtandao wao kuwa wanaume wanaotahiri hawapati ukimwi kwa urahisi. Katika mitandao hio kumeandikwa pia kutopata ukimwi baada ya wanaume kutahiri ni  kwa asilimia 60. Kutokana na mpango wa shirika la afya duniani WHO asili mia 90 ya wanaume Afrika wa umri kati ya miaka 20 hadi 29 wanatakiwa kutahiriwa kufikia mwaka 2021. Pia mvumbuzi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates anaunga mkono kampeni hii.           

"Hii ni changamoto kubwa lakini mwisho kuna faida yake," alisema Bill Gates katika mkutano wa kimataifa wa ugojwa wa ukimwi mjini Durban, Afrika ya kusini mwaka jana.

Ulrich Fegeler ambaye ni mwanachama wa shirikisho la chama cha madaktari cha watoto na vijana, hakubaliani na takwimu zilitolewa na shirika la afya duniani, WHO. Daktari huyo  amesema hakuna umuhimu wa kuwatahiri watu kwa ajili ya kinga ya magonjwa. Amesema kitendo hicho hakiendani na haki za binadamu.

"Watoto wanatahiriwa bila ya kupigwa shindano ya ganzi. Ujerumani kitendo hicho ni marufuku, " alisema Ulrich Fegeler.

Vigezo vya WHO kwawale wanaotahiriwa

Kwa mujibu wa muongozo wa shirika la afya duniani WHO wanaotahiriwa ni wale tu wanaoamua wenyewe na kukubali kutahiriwa kwa ajili ya kinga ya ukimwi. Kutahiriwa pia kufanywe kwa njia ambayo inatumia vyombo safi na wataalamu.

Lakini kwa mujibu wa mwanaharakati Mabola, anasema vigezo hivi havifuatwi. Wawakilishi wa mashirika hayo ya afya kwa anasema Mabola wanashirikiana na walimu wa shule na kuwaambia watoto kuwa wakitahiriwa kawatapata ukimwi au ugojwa wa saratani.

"Mashirika mengine wanawapa watoto pipi,vitu vya kuchezea au pesa. Halafu wanawapeleka katika sehemu za kutahiriwa," alisema Mabola. Mabola aliongezea kusema pia kuwa hakuna utafiti uliofanya wa kuonyesha kweli kutahiri kunatuia magojwa ya ukimwi na saratani. Lakini hakuna utafiti wa aina yoyote.

 

Pia Kennedy Owino kutoka Kenya wa shirika la "Intact Kenya" anasema pia yeye yamtokea haya katika familia yake. Mtoto wa kaka ametahiriwa 2014 bila ya kuulizwa wao au bila yao kutoa ruhusa. Alisema Owino. "Si mama wa mtoto wala bibi alitia saini ya kukubali kitendo hicho. Nilipokutana na kijana huyo hakuweza kujibu mwaswali yoyote. Alikuwa akilia tu," alisema Owino.

Daktari kutoka Austria Jutta Reisinger ameshuhudia watoto wanaume wakitahiriwa katika kituo kimoja nchini Kenya.Wazazi wa watoto hao hawakuarifiwa, alisema Reisinger. Katika kituo hicho pia alishuhudia jinsi gani watoto hao walivokuwa wakiogopa waliposikia wenziwao wakipiga kelele. daktari huyo alisema kuwa watoto hao walikuwa na woga mkubwa.

Kwahiyo wanaharakati wanataka mageuzi makubwa juu ya sera  hii ya kuwatahiri watoto na wanaume kwa ajili ya kinga ya ugonjwa wa ukimwi.

Maloba amesema Uganda inamafanikio makubwa ya  kupigana na ugojwa wa ukimwi kwa kutumia njia ya ABC FORMEL. ABC inasimama kwa  Abstain Be Careful yaani Tunaonya kuwa Makini. Daktari wa watoto pia Ulrich Fegeler anasema njia kama hizo zinazozumiwa Uganda zinasaidia zaidi kupambana na ugonjwa wa ukimwi.

Mwandishi: Daniel Pelz
Tafsiri: Najma Said
Mhariri: Iddi Ssessanga