1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukosefu wa kazi Ujerumani umepungua mno tangu 1949.

2 Machi 2007

Kustawi kwa uchumi kumepunguza mno ukosefu wa kazi Ujerumani.hii ni kwa muujibu wa taarifa za jana za Idara ya Leba kwa mwezi uliopita wa Februari.

https://p.dw.com/p/CHIz

Kustawi kwa uchumi kunakoendelea pamoja na majira yasio ya baridi kali ,kumeongoza kupungua mno kwa ukosefu wa kazi kuliko wakati wowote tangu 1949.Idara ya Leba ya Ujerumani,ilitangaza jana kwamba ukosefu wa kazi mwezi nuliomalizika wa Februari, umepunmgua na kufikia milioni 4.2.

Hii ina mana watu 826.000 walipata kazi mwezi uliopita ukilinganisha na kipindi sawa na hicho cha mwaka uliotangulia.Kwa taarifa hizo za kupendeza,Idara ya kazi ya Ujerumani, inatarajia ukosefu wa kazi mwaka huu kupungua mno.

Mwaka mmoja tu Ujerumani katika soko la ajira ikionekana ni mgonjwa anaeugua miongoni mwa nchi za Ulaya.Hali sasa imegeuka na katika mikoa mbali mbali kuna manun’guniko kwamba kuna ukosefu wa wafanyikazi wenye ujuzi unaotakiwa.sababu ya hali hii ni kuwa kustawi kwa uchumi kumeacha alama yake katika soko la kazi.Ujerumani iliokua ikiugua muda mrefu barani Ulaya katika ukosefu wa kazi imegeuka sasa gurudumu linalosukuma mbele kufufuka uchumi barani Ulaya.Muhimu zaidi ni kuwa,uchumi unapanuka,idadi ya waajiriwa inapanda na idadi ya wasio na kazi inapungua.

Muhimu hapa sio tu kuzidi nafasi za kazi ndogo-ndogo-mini jobs-bali hata kazi kubwa kubwa zinazochangia katika mfuko wa malipo ya bima za jamii.Kumechomoza uhuru zaidi wa kuongezeka masaa ya kazi.Tangu 2003 masaa ya kazi viwandani yalikuwa masaa 58 kwa wiki sasa yamepanda hadi 64 kwa wiki.Viwanda navyo vimeitumia miaka ya misukosuko kuvileta vivanda vyao katika muundo wa kisasa na kwa utandawazi.Viwanda vimeimarika zaidi leo hii kuliko ilivyokuwa miaka michache nyuma.Uwezo wa kushindana na mataifa mengine ya kiuchumi ni mkubwa zaidi leo kuliko ilivyokuwa.

Bila shaka kuwa na watu wasio na kazi kiasi cha milioni 4.2 ni idadi kubwa.Lakini kuwapatia watu 826,000 nafasi za kazi na kuteremsha idadi ya wasio nazi kwa adiri hiyo kuliko ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita yafa kupewa heko.Wataalamu wa taftishi za sayansi ya soko la kazi wanatumai ukosefu wa kazi mwaka huu utateremka na kufikia milioni 3.6 kutoka kima cha sasa cha milioni 4.2.

Kuna upande mwengine wa sarafu: Hata zikifurahisha vipi taarifa hizo nzuri,kuna pia ya kulalamika: Kustawi huku kwa soko la kazi na uchumi kumetokana zaidi na wafanyikazi wenye ujuzi na elimu waliokuwa talari kuhamia sehemu nyengine kufanya kazi.

Wafanyikazi wagonjwa au wasioelimika sana bado wanakumbana na shida kupata kazi nchini Ujerumani.Licha ya kuwapo nafasi za kazi 850,000,idadi ya wanaosaka kazi kwa muda mrefu sasa iliongezeka mwezi wa Februari uliopita.Hii ina maana kinga bora ya kutojikuta huna kazi ni kuwa na kuwa umesomea kazi fulani ya kutegemeka.Kwa bahati mbaya lakini, kiasi cha 10% ya vijana walioacha shule wanashindwa kupata nafasi za kusomea kazi. Kundi hili, ndiko wasio na kazi wa kesho,watatoka na kuomba msaada wa ruzuku.