1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine na Uingereza zatia saini makubaliano ya ushirikiano

Tatu Karema
10 Aprili 2024

Ukraine na Uingereza zimetiliana saini makubaliano ya kushirikiana katika sekta ya ulinzi na utengenezaji silaha hii ikiwa sehemu ya juhudi za wakati wa vita za kuimarisha viwanda vya ndani vya silaha Ukraine

https://p.dw.com/p/4edIk
Greg Hands
Waziri wa sera za kibiashara wa Uingereza, Greg HandsPicha: Michal Wachucik/empics/picture alliance

Makubaliano hayo yalitiwa saini wakati wa kongamano la kijeshi mjini Kyiv lililohudhuriwa na kampuni 30 za ulinzi za Uingereza.

Baada ya hafla ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo, waziri wa viwanda vya kimkakati vya Ukraine Oleksandr Kamyshin, aliwaambia waandishi wa habari kwamba hayo yalikuwa makubaliano ya kwanza ya ushirikiano baina ya serikali.

Shambulizi la droni lashambulia kinu cha nyuklia Ukraine

Kwa upande wake, afisa mkuu mtendaji wa kitengo cha zana za ulinzi na msaada cha Uingereza Andy Start amesema sasa wanatambua kuwa wanahitaji kuimarisha ushirikiano na sekta ya ulinzi ya Ukraine kuiweka katika nafasi bora na kusaidia uchumi wa Ukraine.

Greg Hands, waziri wa sera za kibiashara wa Uingereza, amesema anatumai makubaliano hayo yataleta mafanikio kwa Ukraine katika uwanja wa vita.