1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yadai kuzuia mkururo wa mashambulizi ya Urusi

29 Aprili 2024

Ukraine imedai kuwa imezuia mashambulizi 55 ya Urusi katika eneo la mashariki la Donetsk, siku moja baada ya kukiri kuwa hali ilikuwa mbaya zaidi katika mstari wa mbele wa vita.

https://p.dw.com/p/4fI8O
Wanajeshi wa Ukraine walio mstari wa mbele kwenye vita na Urusi.
Wanajeshi wa Ukraine walio mstari wa mbele kwenye vita na Urusi.Picha: Wolfgang Schwan/Anadolu/picture alliance

Jeshi la Ukraine limesema limefanikiwa kuzuia mashambulizi ya Urusi katika vijiji kadhaa vya kaskazini na magharibi mwa Novobakhmutivka, kijiji ambacho Moscow imedai udhibiti.

Vikosi vya Moscow vimekuwa vikipata mafanikio zaidi katika mkoa wa Donetsk, lakini Ukraine imedai kuwa inaendelea kupambana na adui.

Kamanda mkuu wa jeshi la Ukraine Oleksandr Syrsky amesema hapo janakuwa wanajeshi wake wamerejea kwenye safu mpya za ulinzi katika maeneo ya magharibi. Hata hivyo Kyiv imeonya kuwa Urusi itajaribu kupata ushindi kabla ya kuadhimisha siku ya Uzalendo Mei 9.