1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Ukraine yaihimiza Ujerumani kuipatia makombora ya Taurus

Lilian Mtono
22 Februari 2024

Meya wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Vitali Klitschko ameisifu Ujerumani kwa kuwapatia misaada ya kijeshi hadi sasa, lakini akasema sasa ni wakati kwa Kansela Olaf Scholz kuipatia Ukraine makombora ya masafa marefu.

https://p.dw.com/p/4cjfr
Kyiv, Ukraine | Meya Vitali Klitschko,
Meya wa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, Vitali KlitschkoPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

 

Katika mahojiano ya hivi karibuni na shirika la habari la DPA, Klitschko amesema kwamba moja ya masuala muhimu kwa taifa lake ni iwapo Ujerumani itawapatia makombora waliyoyaomba aina ya Taurus ambayo watayatumia kwa ajili ya kulilinda taifa lao na kuharibu vifaa vya kijeshi vya Urusi.

Ukraine iliiomba Ujerumani makombora ya Taurus yenye uwezo mkubwa na zinazokwenda umbali wa kilomita 500 mwezi Mei mwaka uliopita.

Soma pia:Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani ambebesha dhamana rais wa Urusi kuhusu vita vya Ukraine

Lakini Kansela Scholz hadi sasa amezuia upelekwaji wa makombora hayo nchini Ukraine kwa wasiwasi kwamba yanaweza kutumika kushambulia maeneo tete ya Urusi na kusababisha mvutano zaidi kati ya Ujerumani na Urusi.