1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yasonga mbele na mpango wake wa amani

14 Januari 2024

Wanadiplomasia waandamizi wakutana Davos, kujadili mpango wa amani wa Ukraine . Katika ufunguzi wa mkoutano huo rais Volodymyr Zelensky aliwakilishwa na mkuu wake wa watumishi Andriy Yermak

https://p.dw.com/p/4bE4f
Schweiz, Davos | Ukraine Friedenskonferenz
Picha: Gian Ehrenzeller/POOL/KEYSTONE/picture alliance

Ukraine inasonga mbele na mpango wake wa amani kwa lengo la kuvimaliza vita na Urusi vya karibu miaka miwili sasa. Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa aahidi kuiunga mkono Ukraine

Mpango huo utajadiliwa kwenye mkutano wa maafisa wa usalama wa taifa, kutoka duniani kote unaofanyika kwenye kitongoji cha burudani cha Davos nchini Uswisi.Zelenskiy asema usitishaji mapigano Ukraine utainufaisha tu Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, aliyepangiwa kuhutubia kongamano la kiuchumi la Dunia (WEF) huko Davos hakuwapo kwenye kikao cha ufunguzi leo asubuhi, kilichowaleta pamoja washiriki zaidi ya 80 kutoka nchi na mashirika ya kimataifa.

Zelensky aapa kulipiza mashambulizi yaliyofanywa na Urusi  

Zelensky aliwakilishwa na mkuu wake wa watumishi Andriy Yermak kwenye kikao hicho kilichohudhuriwa pia na mwakilishi maalum wa Marekani, Penny Pritzker anayeshughulikia ufufuaji wa uchumi wa Ukraine.

Ukraine-Vita - Kiev
Kushoto: Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwakilishi maalum wa Marekani, Penny Pritzker anayeshughulikia ufufuaji wa uchumi wa Ukraine.Picha: Ukrainian Presidential Press Office/AP/dpa/picture alliance

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, James O`Brien, anayeshughulikia masuala ya Ulaya na bara Asia, pia alihudhuria mkutano huo.