1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yatakiwa kuelekeza mustakabali wao

29 Januari 2014

Wahariri wameangazia zaidi hii leo kuhusu hali nchini Ukraine , mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi pamoja na mipango ya mafao ya uzee ya serikali ya mseto mjini Berlin.

https://p.dw.com/p/1Aysn
Ukraine Protest in Kiew 28.01.2014
Picha: Reuters

Tukianza na gazeti la Stuttgarter Zeitung kuhusu hali nchini Ukraine linazungumzia kuhusu sera za Umoja wa Ulaya kuelekea Ukraine, Gazeti linaandika.

Watu wa Ukraine wanapaswa binafsi kuamua wapi wataielekeza nchi yao, upande wa mataifa ya magharibi ama mashariki ama ikiwezekana kuwa na uhusiano wa ujirani mwema na pande zote mbili. Katika hilo hata hivyo ni iwapo Umoja wa Ulaya utamkubali ama kumkataa , Vladimir Putin. Ni kiongozi huyo wa Urusi , kwa sera zake za kiuchumi zenye mikakati ya ukandamizaji , ambazo zimeilazimisha Ukraine kujiepusha na mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya na kuzusha wimbi la maandamano ya kutaka kuhusiana na mataifa ya magharibi.

Mtu anaweza kuelewa, lakini haitoshi, wakati mataifa ya Ulaya yanajiingiza katika kuzuwia kila fursa za ndani za Ukraine kutoka kwa kiongozi huyo wa Urusi. Pia hakuna fursa za pamoja za kimkakati kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya, ambazo zinapatikana zitakazosababisha kuiondoa nchi hiyo katika himaya ya Urusi.

Bado tukiwa katika mada hiyo gazeti la Neue Osnabrüker Zeitung linaandika.

Hali nchini Ukraine ni sawa na utaratibu wenye ncha nyingi. Kwanza : Viktor Yanukovich anaweza kupendekeza anachotaka. Waandamanaji wanakata kiongozi huyo aondoke madarakani. Pili : Kwa hali halisi , Umoja wa Ulaya si sehemu ya kutoa malezi kama vile rais wa Urusi Vladimir Putin kwa nchi hiyo. Tatu : Vitali Klitchko anaonesha picha ya upinzani wa mataifa ya Ulaya. Pekee katika ngazi za uongozi yeye anasimama nafasi ya pili, kama sio ya tatu. Nne : Janukovich hatawali kama dikteta. Wanaoifahamu nchi hiyo kiundani wanasema , kwamba anaweza kushinda uchaguzi hata ikiwa utafanyika leo. Pengine ingekuwa bora kutafakari , juu ya kupunguza mbinyo wa kimataifa , kuliko kuanza kama inavyotakiwa kuuongeza. Ama kuanza kuuelekeza upinzani kuchukua mwelekeo wa wastani, ili kuweza kufikia hatma iliyobora.

Katika mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi, gazeti la Saabrücker Zeitung linasema kuwa pande hizo mbili ni lazima zipate wasaa wa kuzungumza baina yao. Mhariri anasema.

Mataifa ya ulaya yanahitaji sera mpya kuelekea mataifa ya mashariki, kwa kuwa kunahitajika ushirikiano badala ya kujaribu kuharibu maslahi na udhabiti nchini Urusi. Urusi kwa upande wake inapaswa kuachana na picha ya uadui kwa Umoja wa Ulaya, ambayo kila wakati inaonesha kuwa mataifa ya Ulaya yana nia ya ukabaila. Kwa upande wake Urusi inakosa mtazamo wa msingi wa kidemokrasia. Putin anapaswa taratibu kutambua kuwa Umoja wa Ulaya si uongozi ambao unaweza kuukaribia wakati unakanyaga haki za binadamu.

Nalo gazeti la Handelsblatt linalochapishwa mjini Düsseldorf linaelezea kwamba Umoja wa Ulaya haujafanikiwa kuweka uzito wake halisi katika uhusiano kati yake na Urusi kutokana na kuliendea suala hilo kwa tahadhari mno. Gazeti linaandika.

Umoja wa Ulaya unajikuta katika mzunguko wa mizozo na kutokana na utendaji kuipatia nchi hiyo fedha nyingi. Ndio sababu Umoja wa Ulaya inahitaji kufanya mazungumzo ya kina na Urusi kuhusu Ukraine nchi ya pili kwa ukubwa katika eneo la bara la Ulaya ili iwe na uthabiti , kuzuwia umwagikaji wa damu na kuzuwia kuporomoka kwa nchi hiyo.

Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung linaandika kuhusu mipango ya serikali ya mseto kuhusu mageuzi ya mafao ya uzeeni. Gazeti linaandika.

Serikali ya mseto katika ajenda yake kuu ya mafao ya uzeeni kwa akina mama imetumbikia katika hali mbaya ya mbinu ya uchaguzi. Pia chama cha SPD kitafaidika na mada yake ya wafanyakazi kustahili kupata mafao ya uzeeni wakiwa na umri wa miaka 63. Hata hivyo lengo ya kustaafu na mapema bado ni la hivi karibuni kabisa. Watu wanahitaji kupata watoto wengi zaidi, na wafanyakazi wanapaswa wahakikishiwe kupata kipato cha juu. Na pia kuna mpango wa kansela Merkel wa kustaafu katika umri wa miaka 67 ambao unahitajika kuidhinishwa. Watu watakuwa wazee na watapata mafao yao kwa muda mrefu, kwa hiyo hapa kunahitajika uwiano kati ya vizazi. Lakini viongozi kutokana na malengo ya kupata kura katika uchaguzi wanashindwa kujizuwia. Vijana wanatakiwa kufanya nini, wakati wengi wao hawataki kusikia kabisa suala hilo la mafao ya uzeeni.

Kwa maoni hayo ndio tunafikia mwisho wa udondozi wa yale yaliyoandikwa katika magazeti ya Ujerumani hii leo.

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman