1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Ulaya na Brazil kuhitimisha makubaliano ya kibiashara

Saumu Mwasimba
13 Juni 2023

Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya,Ursula von der Leyen amesema Umoja huo unataraji kukamilisha,kufikia mwishoni mwa mwaka huu, makubaliano ya kibiashara yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu,

https://p.dw.com/p/4SWoA
Brasilien  Ursula von der Leyen bei  Lula
Picha: Fabio Rodrigues-Pozzebom/Agência Brasil

Von der Leyen aliyeko ziarani katika kanda ya Amerika Kusini,jana huko Brazil alikutana na rais Luiz Inacio Lula da Silva ambaye alikosoa kipengele kilichoongezwa na Umoja wa Ulaya katika mkataba huo, kutokana na wasiwasi wao juu ya kuharibiwa kwa msitu wa Amazon. Von Der Leyen amesema Umoja wa Ulaya unataka kusaidia juhudi za kuusimamia msitu huo.

Mkataba wa kibiashara kati ya Ulaya na Brazil,Argentina, Paraguay na Uruguay,umekwama tangu mwaka 2019 kutokana na wasiwasi  wa Umoja wa Ulaya kuhusu msitu huo

Von der Leyen pia alitangaza msaad wa euro bilioni 2 kwa Brazil, kwa ajili ya kusimamia uzalishaji wa nishati ya Hydrogen isiyochafua mazingira,huku akisifu uongozi wa rais Lula kuhusu sera yake ya mazingira  na mpango wake wa kusitisha hatua ya kukatwa miti katika msitu wa Amazon kufikia mwaka 2030.