1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulemavu barani Afrika unamaanisha nini?

3 Desemba 2016

Kwa Afrika kuwa mlemavu, inamaanisha maisha ya taabu na huzuni, leo ikiwa ni siku ya walemavu duniani, wengi hawawezi kupata elimu na hata kazi. Je misaada ya kimaendeleo inaweza kuleta mabadiliko?

https://p.dw.com/p/2TeWN
Afrika Albinismus
Picha: Getty Images/AFP/T. Karumba

Katika umri mdogo sana Jemimah Kutata alijifunza kupambana na tabia hii mbaya.

"Kwenda shule Afrika kwa mtu ambaye ana ulemavu ni ndoto kwa sababu wavulana wanapewa nafasi ya upendeleo, kwa hiyo ukiwa mwanamke, mwenye ulemavu hilo ni janga mara mbili" anasema Jemimah

Kuhudhuria shule ya msingi halikuwa swali la kujiuliza kwa Kutata pamoja na kuwa wazazi wake walimtaka aweze kupata elimu. Akiwa ni mtu wa kutegemea magongo mawili na kifaa maalum kwenye mguu wake wa kulia kinachomsadia kutembea ilimaanisha kuwa hangeweza kutembea umbali mrefu.

Kwa bahati nzuri wazazi wake walimpeleka katika shule ya bweni, lakini alipopata ajira kwa mara ya kwanza baadaye aligundua tena kwa mara nyingine inamaanisha nini hasa kuishi na ulemavu. Kutata anasema "Siku hizo mtu mweye ulemavu ilikuwa inachukua miaka kupandishwa cheo kwa sababu unaonekana kama ni mtu mgonjwa vile, uko katika meza yako na huwezi kuwa katika nafasi ya maneja."

Lakini licha ya kukumbana na changamoto hizo Jemimah Kutata ni mmoja kati ya walemavu wenye hali nzuri. Karibu asilimia 10 ya watoto wote wenye ulemavu barani Afrika wanahudhuria shuleni na karibu asilimia 80 ya watu wazima wenye ulemavu barani humo hawajaajiriwa. Kwa wengi hii inamaanisha maisha ya umasikini, taabu na kutengwa.

Sheria na miradi ya kuwasadia walemavu yakosolewa

Facundo Chaves Penillas, ni mshauri wa masuala ya haki za binadamu na ulemavu kutoka ofisi ya halmashauri kuu ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikila haki za binadamu, anasema suala la watu wenye ulemavu barani Afrika ni tata na lina changamoto nyingi kama vile rasilimali, miundombinu,na katika mazingira mengine changamoto za kisiasa ambazo zinazuia nchi kuendelea kwa kasi na pia kuna masuala ya dini yanahusika.

Nchi nyingi za kiafrika zimetambulisha sheria kusaidia watu wenye ulemavu lakini kumekuwa na upungufu wa pesa kwa ajili ya kufanyia utekelezaji sheria hizo.

Ein Albinokind in Abuja in Nigeria Afrika
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kutoka Abuja nchini NigeriaPicha: picture-alliance/ dpa

"Masuala mengi yana uhusiano na maendeleo na swali ni kuwa je ni jinsi gani nchi zinaweza kumudu huduma za muhimu na mabadiliko yanayotakiwa," aliongeza Penillas

Miradi mingi ya maendeleo imeshindwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu wakati kifungu cha 32 cha mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu kinawataka kufanya hivyo. Mkataba huo umeanza kufanya kazi miaka 10 iliyopita lakini mabadiliko yanachanganya.

"Bado tuna njia ndefu ya kufika tunakoelekea, mipango ya kimataifa inahitaji kuwa na utaratibu ambao utawajumuisha watu wenye ulemavu," anasema Kutata mkenya ambaye ni mlemavu.

Hans- Joachim Fuchetel mbunge na katibu wa dola katika Wizara ya ushirikiano na maendeleo ya Ujerumani anasema Ujerumani imepanua mipango yake na kusema kuwa sasa wana miradi zaidi ya 40 katika nchi zaidi ya 20, na kuongeza kuwa Wizara inafanyia kazi mkakati mpya ambao inajumuisha mahitaji ya watu wenye ulemavu.

"Ujerumani haiko juu ya nchi ambazo zinafanya utekelezaji wa kifungu cha 32 lakini inaweza kujifunza mengi kutoka nchi nyingine" anasema Theresa Degener Profesa wa sheria ambaye alisaidia katika kuandika mkataba huo.

Jemimah Kutata amejifunza mengi kutoka katika harakati ambazo zimemjengea heshima katika maisha yake, kwa sasa anaendesha taasisi ya kifedha ambayo husaidia watu wenye ulemavu katika eneo la Pwani ya Kenya ikiwa ni muungano wa watu wenye ulemavu wa Kenya.

Kutata anasema, " Washiriki wengi sasa wanaweza kupata chakula, lakini najisikia kuwa bado kuna vitu zaidi vinahitajika kufanywa kwa walemavu kufahamu haki zao.

Mwandishi: Celina Mwakabwale

Mhariri:Josephat Charo