1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu unahitaji fikra na mawazo mapya

18 Desemba 2009

Majadiliano ya kimataifa huwa magumu hasa panapokuwepo maslahi ya kitaifa. Kwa hivyo, waasisi wa sera za kimataifa za hali ya hewa wanatanguliza hoja za kisayansi na kiuchumi katika majadiliano yao mjini Copenhagen.

https://p.dw.com/p/L736
A handout image released by the Danish Foreign Affairs Ministry shows Britain's Prince Charles during the welcome ceremony at the COP15 United Nations (UN) World Climate Conference in Copenhagen, Denmark, 15 December 2009. The conference runs through 18 December 2009 and entered its decisive phase. EPA/DANISH FOREIGN AFFAIRS MINISTRY / HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mwanamfalme Charles wa Uingereza.Picha: picture alliance / dpa

Wote wamekwenda Copenhagen kwa nia nzuri. Kuanzia wageni wa heshima,viongozi wa serikali na nchi,wajumbe wa mashirika yasio ya kiserikali, makampuni, Umoja wa Mataifa, wanaharakati wa mazingira hadi vijana ,wachumi na wanasayansi.

Katika ufunguzi rasmi wa kikao cha mawaziri kwenye mkutano huo wa hali ya hewa mjini Copenhagen, Mwanamfalme Charles wa Uingereza alisema:

" Mfumo unaohifadhi maisha katika sayari yetu unapoanza kwenda kombo na kuendelea kuishi kwetu kunatiwa mashakani, basi kumbukeni kuwa watoto na wajukuu wetu hawatouliza kile kilichotamkwa na kizazi chetu bali watataka kujua tulichokifanya. Kwa hivyo tuwape jawabu la kuweza kujivunia."

Ni dhahiri kuwa kila mmoja wetu anataka kuihifadhi dunia dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa - lakini suali ni vipi? Mwenyekiti wa IPCC- baraza la wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya hali ya hewa, Rajendra Pachauri anasema madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yanajulikana kote - katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Lakini uwezekano wa kuathirika hutegemea madhara yanayokabiliwa, maendeleo ya nchi na hatimae maliasili na uwezo wa jamii kujirekebisha kuambatana na mabadiliko ya hali ya hewa. Kwa hivyo ni dhahiri kuwa kote duniani, masikini ndio wanaokabiliwa zaidi na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Rajendra K. Pachauri, chairman of the "Intergovernmental Panel on Climate Change" speaks to youth organizations at the UN Climate Summit in Copenhagen on Monday, Dec. 14, 2009. (AP Photo/Polfoto,Tariq Mikkel Khan) ** DENMARK OUT **
Mwenyekiti wa IPCC, Rajendra K.Pachauri.Picha: AP

Nchi nyingi zinazoendelea na hata mashirika yasio ya kiserikali yanaamini kuwa mfumo wa kiuchumi duniani unahitaji kufanyiwa mageuzi. Hiyo amesisitiza Kumi Naidoo alie mwenyekiti wa Greenpeace International -shirika linalogombea mazingira. Yeye anasema, mtu anapokabiliwa na mzozo mkubwa, tatizo hilo haliwezi kutenzuliwa kwa fikra,taasisi na mawazo yale yale ambayo yalisababisha mzozo wenyewe. Mtu anapaswa kufikiria upya na vingine. Kwa hivyo Kumi Naidoo anawataka wajumbe wa hadhi ya juu mkutanoni Copenhagen walio na hatima ya wanadamu mikononi mwao, wafikirie njia mpya za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ikiwa makubaliano ya kupunguza utoaji wa gesi zinazochafua mazingira yatapatikana sasa, basi gharama zake zitakuwa ndogo kuliko vile ilivyodhaniwa hapo awali. Vile vile kuna faida nyingine, amesisitiza mwenyekiti wa IPCC, Rajendra Pachauri. Kwa mfano anasema, mabadiliko katika sekta ya nishati yatasaidia kutoa nafasi mpya za ajira na kuvutia uwekezaji. Vichocheo hivyo pekee vinatosha kuyavutia mataifa tajiri yenye viwanda kwa maslahi yao wenyewe.

Mwandishi:H.Jeppesen/ZPR/P.Martin

Mhariri: M.Abdul-Rahman