1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu waomboleza na kumuenzi Mandela

6 Desemba 2013

Ulimwengu unahuzunika kutokana na kifo cha Nelson Mandela,kiongozi mashuhuri aliyeingia katika madaftari ya historia ya karne ya 20 kama "chimbuko la kuwapa watu moyo wa kuthamini maadili,kusamehe na kusikilizana.

https://p.dw.com/p/1AUAT
Nelson Madiba MandelaPicha: Reuters/Mike Hutchings

Msiba umetanda kote ulimwenguni tangu zilipotangazwa habari za kifo cha Nelson Mandela.Bendera zimeshushwa nusu milingoti katika kila pembe ya dunia.Na Siku hadi tatu za maombolezi kutangazwa katika nchi nyingi duniani.Viongozi wa kimataifa wameelezea masikitiko yao na kusifu mchango wa Madiba kama mtu aliyekuwa akipigania haki,uhuru na usawa ulimwenguni.Rais Barack Obama wa Marekani anasema kwa kufariki dunia Nelson Mandela,ulimwengu umempoteza mmojawapo wa binaadam mwenye ushawishi mkubwa kabisa,mwenye moyo wa kijasiri kupita kiasi na mwenye imani kupita kiasi.Rais Obama ameungama maisha yake yasingekuwa kama yalivyo ingekuwa dunia haijakuwa na mpinzani wa zamani wa Afrika kusini aliyetumikia miaka 27 jela.Rais Barak Obama amenukuu yale yaliyosemwa na Madiba alipofikishwa mahakamani mwaka 1964 "Nimepigana dhidi ya utawala wa kimabavu wa waupe na nimepigana dhidi ya utawala wa kimabavu wa watu weusi.Nnapigania maadili ya kuwepo jamii huru na ya kidemokrasia ambapo watu wote wataishi pamoja kwa furaha na kuwa na fursa sawa.Ni Maadili nnayotaraji kuyaendeleza maishani mwangu na ikihitajika basi pi niko tayari kufa kwaajili ya maadili hayo."

Hikma,Busara na moyo wa imani ndizo sifa zake

Matamshi kama hayo yaetolewa pia na kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliyesema jina la Nelson Mandela daima litafungamanishwa na mapambano ya wananchi wa Afrika kusini dhidi ya unyonyaji na kupinduliwa utawala wa ubaguzi wa rangi na mtengano Apartheid.Miongo zaidi ya miwili jela haikumbadilisha Nelson wala haikumtia chuki moyoni.Afrika kusini mpya imeibuka kutokana na wito wake wa suluhu."Amesema kansela wa Ujerumani Angela Merkel.

Stimmen und Reaktionen zum Tod Nelson Mandelas
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ban Ki-moon akitoa rambi rambi zake kwa kifo cha Nelson MandelaPicha: Reuters/Mark Garten

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amemtaja Nelson Mandela kuwa ""Mtu asiyekuwa na mfano katika kupigania haki.Hakuwa na kinyongo.Ameonyesha kinachowezekana kutendeka katika dunia na katika kila mmoja wetu anasema katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon,aliyetoa nasaha watu wawe na imani na kushirikiana kwaajili ya kupigania haki na utu.

Amerika kusini rais wa Brazil Dilma Roussel amemtaja Nelson Mandela kuwa "mtu mashuhuri mwenye ushawishi mkubwa kabisa wa karne ya 20.Amesema Nelson Mandela ameongoza utaratibu wa maendeleo katika historia ya binaadam kwa busara na mapenzi-utaratibu uliopelekea kumalizika enzi za ubaguzi wa rangi na mtengano.

Malkia Eliabeth wa pili wa Uingereza pia ameelezea masikito yake kutokana na kifo cha Nelson mandela akisifu juhudi zake .Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza anasema tunanukuu:"Juhudi zake ndizo zilizopelekea kuwepo Afrika kusini yenye amani hii leo.

Na waziri mkuu wa Uingereza David Cameroun anasema:"Nelson Mandela hakuwa shujaa wa wakati mmoja tu ni shujaa wa enzi zote."

Amefuata nyayo za Gandhi

Waziri mkuu wa India ,Manmohan Singh amemtaja Nelson Mandela kuwa kiongozi aliyefuata kweli nyayo za Mahatma Gandhi.

Stimmen und Reaktionen zum Tod Nelson Mandelas
Watu wanaomboleza na kumlilia Nelson MandelaPicha: Reuters/Siphiwe Sibeko

Sifa na maombolezi yametolewa pia na viongozi wa Ufaransa,Australia,Mashariki ya kati na Latin Amerika kusifu mchango wa Nelson Mandela nchini mwake na ulimwenguni.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Rduters/AFP

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman