1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulinzi waimarishwa Ubelgiji kwa hofu ya kutokea shambulio la Kigaidi

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cerw

BRUSSELS.

Wakuu wa usalama wa Ubelgiji wanasema wameimarisha ulinzi katika mji mkuu wa Brussels- kufuatia hofu ya uwezekano wa kukatokea shambulio la kigaidi. Tangazo limekuja baada ya polisi wa Ubeligiji kusemekana kuwakamata watu 14 ambao inasema walikuwa wanapanga kumtorosha kutoka jela raia mmoja wa Tunisia.Mshukiwa huyo alikamatwa mwaka wa 2001 kwa kushtukiwa kupanga kushambulia vituo vya Marekani.Wanausalama wanasema watu waliokamtwa leo walikuwa wanapanga kutumia baruti katika mpango wao huo.Wanaendelea kuhofia kuwa huenda baruti hizo zingetumiwa kwa shughuli zingine,kwa hivyo polisi imeamua kuimarisha ulinzi katika mji mkuu.