1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ULM:UJERUMANI:Hakuna tishio la shambulizi

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhr

Serikali ya Jimbo la Ulm hapa Ujerumani imesema kuwa hakuna hatari yoyote ya shambulizi la kigaidi, baada ya kupatika kwa taarifa za kushambuliwa kwa hospitali ya jeshi.

Hapo jana mtu mmoja alipiga simu polisi akisema kuwa bomu limetegwa katika hospitali ya jeshi iliyoko kusini mwa mji huo wa Ulm.

Hata hivyo baada ya polisi kuwahamisha wagonjwa na wafanyakazi, walifanya upekuzi na hakukuwa na bomu lolote lililopatikana..

Polisi bado hawajaelezea lolote juu ya mtu huyo aliyepiga simu.