1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa na hali ya usalama nchini Burundi

11 Aprili 2014

Umoja wa mataifa umeitahadharisha serikali ya Burundi na kuitaka kuchukua hatua zinazohitajika ili kukabiliana na kuzidi kuzorota kwa hali ya kisiasa na kiusalama.

https://p.dw.com/p/1BgW0
Umoja wa Mataifa wafanya wasiwasi kuhusu usalama nchini Burundi
Picha: Reuters

Naibu Msemaji wa rais Pier Nkurunziza, Wili Nyamitwe amekanusha taarifa zinazosema kwamba serikali imekuwa ikiwapatia vijana wanamgambo wa chama tawala CNDD fDD silaha wanaotajwa na Umoja wa Mataifa kuwa chanzo cha kuzorota kwa usalama. Wili Nyamitwe ni Naibu msemaji wa rais Nkurunziza aliyezungumza na Amida ISSA alikuwa na haya ya kusema. Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amida Issa

Mhariri: Saumu Yusuf