1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa waomba msaada zaidi wa kibinadamu Kongo

Tatu Karema
20 Aprili 2024

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dharura la msaada wa kibinadamu kwa mamilioni ya watu walioathirika kutokana na ghasia katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

https://p.dw.com/p/4f0Le
Wakimbizi wa Kongo wakusanyika katika kambi ya wakimbizi viungani mwa mji wa Goma mnamo Machi 13,2024
Wakimbizi wa Kongo katika kambi ya wakimbizi viungani mwa mji wa GomaPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Mratibu wa msaada wa kibinadamu wa Umoja huo nchini Kongo, Bruno Lemarquis, alisema jana kwamba  kufikia mwezi Aprili, ni asilimia 15 tu ya fedha zinazohitajika kuwasaidia watu milioni 8.7 zilizokuwa zimepatikana na kwamba mahitaji ni makubwa zaidi kuliko wanachoweza kutoa.

Dola bilioni 2.6 za msaada zinahitajika kwa mwaka huu 

Umoja wa Mataifa unahitaji angalau dola bilioni 2.6 kwa mwaka huu, lakini unahofia kuwa kuwepo kwa migogoro mingi duniani kumeufunika mgogoro huo wa Kongo.

Soma pia: Umoja wa Mataifa waonya kuhusu kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama Mashariki mwa Kongo

Mratibu huyo amesema kwa sasa wanalazimika kutoa msaada huo kwa kuzingatia vipaumbele, kutokana na kiwango kidogo cha ufadhili wa shughuli za kibinadamu nchini Kongo katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.