1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wapambana na njaa kwenye Pembe ya Afrika

Abdu Said Mtullya28 Julai 2011

Ndege ya kwanza ya Umoja wa Mataifa yapeleka chakula nchini Somalia .

https://p.dw.com/p/125KZ

Ngede za Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa WFP zimeanza kupeleka chakula nchini Somalia baada ya ndege ya kwanza kutua mjini Mogadishu jana alasiri.

Maafisa wa Umoja huo wamearifu kuwa ndege hiyo ilipeleka tani 10 za kwanza za chakula kwa ajili ya watoto waliokumbwa na utapiamlo. Umoja wa Mataifa pia umefahamisha kwamba katika siku zijazo tani nyingine 70 za chakula zitapelekwa Somalia kwa ndege kutokea Kenya.

Kwa jumla watu milioni11 sasa wanategemea misaada ya chakula. Akizungumzia katika mahojiano na gazeti la Frankfurter Rundschau Kamishna wa serikali ya Ujerumani wa masuala ya Afrika Günter Nooke amesema biashara ya kuizuia China ardhi katika nchi za Afrika pia inasababisha maafa ya njaa. Amesema kuzalisha chakula kwa ajili ya kukiuza nje kunaweza kusababisha migogoro mikubwa ya kijamii barani Afrika.