1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa watoa tahadhari ya njaa inayoongezeka DRC

21 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari siku ya Jumanne kuhusu hali mbaya ya njaa inayoripotiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ukisema kuna uhaba mkubwa wa fedha na rasilimali za kulisaidia taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4WdMm
 WFP statement about looting of it´s  aid in Tigray
Picha: Million Hailesilassie/DW

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema mwaka huu nchini Kongo, takriban watu milioni 25.8 watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. 
       
Msemaji wa WFP Tomson Phiri amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa  kwamba kwa ujumla, wanahitaji dola milioni 870 ili kutoa misaada ya kibinadamu nchini DRC.

WFP: Njaa itaongezeka baada ya ufadhili kupungua

lakini amesema kwa sasa wamepungukiwa na asilimia 85 ya fedha hizo, ikiwa ni sawa na dola milioni 738.5.

Phiri amesema hali ni mbaya zaidi Mashariki mwa Kongo, sehemu inayokumbwa na mgogoro uliosahaulika.