1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA:Mustakabal wa Kosovo uko matatani

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBht

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa linakabiliwa na mgawanyiko kuhusu hatma ya Kosovo baada ya Urusi kupinga rasimu ya azimio la baraza hilo.Azimio hilo linaloungwa mkono na mataifa ya Marekani,Uingereza na Ufaransa linatoa wito wa kufanywa mazungumzo zaidi katika kipindi cha siku 120 kati ya waasi wa Belgrade na Albania kuhusu mustakabal wa Kosovo.Urusi kwa upande wake inashikilia kuwa lengo la azimio hilo ni kuipa Serbia uhuru wake.

Kwa mujibu wa balozi wa Urusi katika Umoja wa mataifa Vitaly Churkin juhusi za mataifa hayo manne zinapokelewa vizuri ila uwezekano wa azimio hilo kutimizwa haupo.

Mpatanishi wa Kosovo katika Umoja wa Mataifa Martti Ahtisaari anapendekeza uhuru wa masharti Fulani kwa jimbo la Serbia huku Belgrade na Urusi zikipinga vikali mpango huo.Mpango huo huenda ukawezesha jimbo hilo kusimamiwa na Umoja wa Ulaya badala ya Umoja wa mataifa.

Hapo jana katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alitoa wito kwa Baraza hilo kutoa uamuzi wa haraka kuhusu mustakabal wa Kosovo.Wakati huohuo Urusi inapendekeza kuondolewa kwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kosovo Martti Ahtisaari.