1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA–NEW YORK:Mustakabal wa Kosovo kucheleweshwa

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpl

Marekani na washirika wake wa Umoja wa Ulaya katika
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamesambaza
waraka wa azimio, litakalochelewesha mabadiliko
kuhusiana na hali ya baadae ya jimbo la Serbia la
Kosovo. Kucheleweshwa huko kwa siku 120 kunalenga kuruhusu mazungumzo yaanze kati ya Serbia na
viongozi wa jamii ya wenye asili ya Kialbania katika Kosovo kuhusu hali ya baadae ya jimbo hilo.

Serbia na
Urusi zinaupinga mpango wa umoja wa mataifa unaopendekeza uhuru kamili kwa Kosovo na Urusi imetishia kutumia kura ya turufu kupinga azimio litakalounga mkono uhuru kwa Kosovo.