1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Nchi zinazosafirisha gesi ya ardhini duniani unaundwa

Miraji Othman24 Desemba 2008

Umoja wa nchi zinazosafirisha gesi ya ardhini hauwezi kuwa sasa na OPEC

https://p.dw.com/p/GMUU
Waziri mkuu wa Russia, Vladimir Putin(katikati), akiwa pamoja na walioshiriki katika mkutano wa nchi zinazosafirisha gesi ya ardhini duniani uliofanyika Mosko, Disemba 23, mwaka huu wa 2008Picha: AP


Hali ya Ulaya kutegemea nishati ya kutokea na kupitia Russia ni ukweli wa mambo. Lakini ni jambo lisilokuwa na msingi kuingiwa na hofu kutokana na na kuundwa umoja wa nchi zinazotoa gesi ya ardhani, mfano kama ule umoja wa nchi zinazosafirisha mafuta duniani, OPEC. Neno GAS-OPEC linaweza kuwa zuri katika kutunga siasa. Ni neno fupi lenye kutoa sauti na la kuvutia, kama kichwa cha habari. Wakati huo huo linatoa sura zaidi ya jumuiya. Kwa mtu wa Ulaya anayekaa katika chumba chake kilicho na ujoto, kutokana na neno hilo, mara anafikiria juu ya uhaba wa kuweko gesi ya ardhini masokoni, jambo ambalo linaweza kufanywa kwa makusudi, na bei ya nishati hiyo maisha kwenda juu, hasa ikiwa jambo hilo litafanyika katika wakati huu wa mizozo.

Na mtu huyo wa Ulaya anapozidi kufikiri na kuziangalia nchi ambazo zitakuweko katika umoja huo, basi huona kwamba mambo yatakuwa mabaya zaidi. Katika umoja huo wa nchi zinazotoa gesi ya ardhini, Iran imo, nayo kwa kawaida hujulikana kuwa ni nchi korofi, au Libya na Venezuela, nchi zilizo na marais ambao sana hujiamulia wenyewe mambo, na, bila ya shaka, jirani mkubwa na asiyetabirika upande wa Mashariki, yaani Russia.

Serekali ya Russia ingependa mtu awe kidogo na hofu nayo. Kwani kuwa na hofu nayo ni kuiheshimu, na heshima ni muhimu kwa Russia, kwani hali hiyo itafanya itambuliwe na iweze kucheza pamoja katika matamasha ya nchi zilizo kubwa na zenye nguvu. Na ndio maana jamii ya kimataifa imegutuka kwa njia nzuri kuundwa umoja huu wa nchi zinazosafirisha gesi, hasa kwa vile nyuma ya sababu ya kuundwa kwake haijajificha, ni tu kuuboresha mfumo wa kabla wa jumuiya hiyo. Jumuiya hiyo sasa itakuwa na makao makuu ya pamoja na sekretariat ya kudumu.

Pindi tukijaribu kufikiria kwamba kweli jumuiya hiyo ya GAS-OPEC itaasisiwa, basi mtu mara atatambua kwamba jambo hilo haliwezekani. Mfano kama wa jumuiya ya nchi zenye kusafirisha mafuta duniani hauwezi kufanya kazi, na jambo hilo linajulikana pia nchi zilizoshiriki katika jukwaa la Gesi ya Ardhini lililofanyika mjini Mosko.

Mfumo wa kimsingi wa OPEC ni kuweka utaratibu wa viwango vya utoaji wa mafuta ili kuwa na ushawishi katika uwekaji wa bei. Jambo kama hilo haliwezi kufanya kkwa katika gesi ya ardhini, na sio tu kwamba bei ya gesi inategemea bei ya mafuta. Kutokana na hali ya usafiri, hakuna soko la gesi ya ardhini duniani linalofanya kazi. Nchi zinazotoa nishati hiyo haziwezi kwa urahisi kupeleka nishati yao kwa njia ya meli au magari, zinabidi zitegemee mabomba, na jambo hilo lina gharama ya fedha nyingi.

Ndio maana Russia bado inapenda kuwa na mikataba ya muda mrefu katika kuuza gesi yake ya ardhini. Kwa mfano, kampuni kubwa la gesi la Russia, Gasprom, limetiliana saini mikataba ya muda mrefu hadi mwaka 2036 au 2046 pamoja na makampuni ya nishati ya Ujerumani, E-On na tawi la kampuni la BASF, Wintershall. Huu ni ukweli unaoonesha mafungamano yalioko, na mazungumzo yote juu ya hatari katika kuundwa jumuiya hii ya Gas-OPEC, angalau kwa sasa, ni jambo la upuuzi.

Na ikiwa uhaba wa gesi hautafanywa kwa makusudi na suala la kupandishwa juu sana bei ya nishati hiyo haliko, mtu anauliza kuna sababu gani ya kuundwa umoja huo? Jee tu kuonesha misuli kuelekea nchi za Magharibi? Sababu kamili sio hiyo. Russia, ambayo inadhibiti asilimia 22 ya soko la gesi ya ardhini duniani, ina hamu ya kuweko maelewano katika masuala ya usafirishaji wa nishati hiyo na sehemu ambazo nishati hiyo itapokelewa. Inataka kuwa na ushawishi kwa nani na vipi gesi yake isafirishwe. Hivyo, Ulaya, ambayo inajaribu kujipatia gesi iasiokuwa na ushirika wa Russia, itaweza kupima na kuamua. Nchi za Ulaya zitaendelea kubakia na mikataba na Russia, kama nchi inayoipatia gesi na pia nchi ambayo inapitia gesi ya kujia Ulaya. Lakini pia Russia ni yenye kutegemea, inajaribu kujihakikishia mustakbali wake kutokana na jumuiya hii ya nchi zinazosafirisha gesi. Serekali ya Russia inajuw akwamba uchumi wa nchi hiyo utaendelea kutegemea mapato ya mafuta. Bila ya kuuza gesi na mafuta yake kwa bei zisizolegalega, nchi hiyo haitoweza kuitekeleza mipango yake yote mizuri ya kutaka kuwa nchi ya kisasa na kujijenga.