1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kushirikiana zaidi

18 Juni 2010

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuwa na kanuni kali zaidi za bajeti na kuratibu sera zao za uchumi katika jitahada ya kudhibiti mzozo wa madeni katika kanda ya Euro.

https://p.dw.com/p/Nu8K
German Chancellor Angela Merkel addresses a news conference about Germany's budget cuts in Berlin, on Monday, June 7, 2010. The German Cabinet has finalized a package of government savings meant to keep the country's debt in check. Chancellor Angela Merkel says the country needs to save a total of 80 billion euro (US dlrs 96 billion) through 2014. (AP Photo/Markus Schreiber
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Kwenye mkutano wao mjini Brussels, viongozi wa taifa na serikali kutoka nchi wanachama 27 wamekubali pia kuchapisha matokeo ya uchambuzi uliofanywa kuhusu benki 25 kubwa kabisa za Ulaya,juu ya uwezo wa benki hizo kukabiliana na mizozo ya kifedha katika siku zijazo.

Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya vile vile wamekubali kuanzisha mpango wa kuzitoza kodi maalum benki za Ulaya. Na katika mkutano wa kundi la nchi 20 zilizoendelea na zinazoinukia kiuchumi, utakaofanywa nchini Kanada baadae mwezi huu, watapendekeza kuzitoza benki kodi kwa kila biashara ya fedha. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema, Umoja wa Ulaya utaimarisha ushirikiano wake. Wanachama wote wametambua kuwa ni lazima kushirikiana zaidi.

Mwandishi:P.Martin/ZPR