1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na Marekani kufanya mkutano maalum wa kiuchumi.

Sekione Kitojo30 Aprili 2007

Rais wa bunge la umoja wa Ulaya Angela Merkel anataka kuzungumza na rais wa Marekani George W. Bush kuhusu uwezekano wa kuwa na umoja wa kibiashara kati ya Umoja huo na Marekani. Siasa za kibiashara zitakuwa ajenda muhimu sana , kwasababu Marekani na bara la Ulaya zinahusika na karibu asilimia 40 hivi sasa ya biashara yote ya dunia.

https://p.dw.com/p/CHFC
Kansela Angela Merkel na rais George Bush wanataka msimamo mmoja kibiashara.
Kansela Angela Merkel na rais George Bush wanataka msimamo mmoja kibiashara.Picha: AP

Hakuna haja ya kukumbatiana , wanatoa ushauri wabunge kadha kwa wawakilishi wa umoja wa Ulaya , ambao wanasafiri leo kwenda Marekani kuhudhuria mkutano huo wa maeneo haya mawili makubwa ya kiuchumi.

Kutokana na hayo kansela na rais wa bunge la Ulaya Angela Merkel pamoja na rais wa kamisheni ya Ulaya Jose Manuel Barroso wanazungumzia kwa matumaini makubwa kutokana na soko kubwa kati ya pande hizo, ambalo litasaidia kukuza uchumi wa maeneo hayo. Hilo litakuwa jibu mujarabu kwa utandawazi, amesema kansela wa Ujerumani kwa ufupi, na hali ya baadaye ya ushirikiano huu wa kiuchumi utazungumziwa zaidi katika mkutano huo mjini Washington.

Ila tu anaona mbunge wa bunge la Ulaya ambaye ni kiongozi wa kundi la kiliberali katika bunge hilo Graham Watson kuwa hali ya kisiasa ya rais wa Bush haileti tija.

O-Ton Watson

Kwa misingi ya maadili ya kiuchumi na ulinzi wa mazingira, serikali ya Marekani imekuwa ikiyumbisha maadili hayo, ambayo Marekani ilikuwa tunaiheshimu. Changamoto kwa mataifa wanachama wa umoja wa Ulaya ni kupinga hatua za Marekani za kufanya mambo kwa matakwa yake. Na hii ni kwamba rais Bush amefanikiwa katika sera zake za kugawa na kuitawala Ulaya, kama alivyo rais Putin.

Umoja wa Ulaya na serikali ya Ujerumani zinatayarisha kwa pamoja mpango wa soko la pamoja , lakini bunge la Ulaya mjini Strassburg linakumbuka mzozo ambao ulikuwapo baina ya umoja huo na Marekani. Tofauti iliyopo katika mapambano ya mabadiliko ya hali ya hewa, masharti ya kuweza kuingia nchini humo, ambapo raia wa umoja wa Ulaya kutoka Ulaya ya mashariki wanavyopata taabu ya kupata viza. Mbinu chafu zinazotumiwa na Marekani katika mapambano yake na ugaidi , haya yote yanaathiri misingi ya haki za bara la Ulaya.

Pamoja na mzozo uliopo hivi sasa wa ujenzi wa ngao ya kinga dhidi ya makombora katika nchi za Poland na jamhuri ya Cheki, suala ambalo limejenga ufa baina ya mataifa ya Ulaya mashariki na magharibi wanachama wa umoja wa Ulaya.

Maeneo haya mawili makubwa kabisa kiuchumi duniani , Marekani na umoja wa Ulaya hata hivyo yanatofauti kubwa sana kiuchumi, lakini rasmi kimkataba hayajaweza kufanikisha.

Ulaya na Marekani ni washirika wakubwa kibiashara duniani. Tunapaswa kuimarisha ushirika huu kati ya maeneo haya mawili. Amesema rais wa kamisheni ya Ulaya Jose Manuel Barroso. Amedokeza Barroso pia kuwa biashara na uwekezaji ndio msingi mkuu wa mahusiano haya ya pande hizi na hali hiyo tunapaswa kuiendeleza.