1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya ulipoanzishwa miaka 50 iliyopita.

Sekione Kitojo22 Machi 2007

Hakutakuwa na vita tena katika Ulaya. Hiyo ilikuwa ahadi baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, wakati umoja wa Ulaya ulipoanza kuundwa. Mwaka 1949 mataifa kumi ya Ulaya ya magharibi yalianzisha baraza la Ulaya. Mataifa hayo yalianzisha katika mwaka 1951 umoja wa Ulaya wa mataifa yanayozalisha mkaa wa mawe na chuma. Ni mazingira gani ya kisiasa na kiuchumi katika miaka ya 50 yalikuwapo kwa mataifa hayo sita katika ule uliojulikana kama mkataba wa Roma mwaka 1957, anaandika Julia Elvers-Guyot.

https://p.dw.com/p/CHHn

Pikipiki za Vespa na magari madogo ya Isetta, katika miaka ya 50 yalikuwa ni alama ya utaifa katika hali ya kuondoka katika vita na mwanzo wa maajabu ya ukuaji wa uchumi. Ukuaji wa pamoja wa uchumi katika Ulaya , umesababisha kila mmoja kujaribu kuzuwia vita vingine katika bara la Ulaya.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Robert Schuman alianzisha mpango wakati huo wa kufanyakazi kwa pamoja katika sekta za uchimbaji wa makaa ya mawe na chuma, ambapo nchi ya Ujerumani inayokaliwa na majeshi ilitaka kuzuwia.Mpango huo kwa ajili ya umoja wa nchi zinazochimba makaa ya mawe na chuma , aliuwasilisha hapo May 9 1950 kwa nchi za Uingereza , Italia, Ujerumani na nchi za Ubelgiji, Uholanzi na Luxemburg zinazotambulika kama nchi za Benelux.

Uingereza, mzalishaji mkuu wa makaa ya mawe na chuma katika Ulaya , ilikataa kutokana na hofu juu ya uwezo wake mkubwa katika sekta hiyo.

Wakomunist waliona uundwaji wa umoja wa nchi zinazotoa mkaa wa mawe na chuma kama mapambano dhidi ya kambi ya mataifa yaliyomo upande wa Urusi ya zamani.

Walishutumu kitendo cha kuiingiza tena Ujerumani ya magharibi katika kambi ya mataifa ya magharibi , ambayo wanaishutumu kwa kujitayarisha kwa vita ya tatu ya dunia.

Kwa hakika iliwakasirisha, lakini kwa upande wa Wakomunist kulitokea vita mpya, vita vya Korea kutoka mwaka 1950 – 53. Vita hivi viliusitua ulimwengu, na rais wa Marekani Harry Truman alikuwa katika mbinyo mkali.

Hatua zilizochukuliwa nchini Korea na wakomunist wadanganyifu zinaonyesha wazi ni jinsi gani misingi yao ya kiutu, ambapo umoja wa mataifa uliasisiwa. Hii ni changamoto kwa mataifa yote yanayopenda amani, kujenga aina ya dunia , ambapo watu wataweza kuishi katika uhuru na amani.

Vita vya Korea viliyafanya mataifa ya Ulaya kuona wazi, ni muhimu kiasi gani , kwao wao pia kuunda umoja wa kiulinzi. Marekani iliwaomba washirika wake, pia juu ya kufikiria kuipatia silaha Ujerumani ya magharibi. Ndipo mwanasiasa mchumi wa Ufaransa Jean Monnet alipounda mpango wa mataifa ya magharibi kujilinda , pamoja na kuishirikisha Ujerumani ya magharibi. Kwa upande wa Ujerumani ya mashariki, utawala wa nchi hiyo ulikuwa unajishughulisha na hali ya machafuko.

Rais wa DDR Wilhelm Pieck katika mwaka 1952 alitangaza kuwa nchi hiyo inajenga Usoshalist.

Wakati katika kila sehemu taifa letu bila kucoka linajaribu kujenga hali ya amani, kundi la watu wahalifu katika eneo la magharibi ambayo ni ardhi yetu iliyoko chini ya majeshi ya Marekani , wanawaelekeza raia wetu wa Ujerumani katika vita vya tatu vya dunia.

Silaha zilianza kupambanishwa, hata katika michezo mapambano ya kinchi yalianza, katika mashindano ya majira ya baridi ya olimpiki mjini Oslo na Helsinki mwaka 1952, na kabla ya hapo.

Machi 5 1953 radio ya Urusi ilitangaza kifo cha Stalin. Miezi michache baadaye vilimalizika vita vya Korea. Kushindwa kwa umoja wa kujihami wa mataifa ya Ulaya kulikuwa mwanzo wa juhudi za kutaka mshikamano, ambao ulifanyika kwa kupitia umoja wa mataifa yanayozalisha mkaa wa mawe na chuma , ambao hapo kabla ulitupiliwa mbali.

Kuundwa kwa umoja wa mataifa ya Ulaya hapo Oktoba 1954 ilikuwa ni hatua ndogo kwa ajili ya umoja wa wachimba migodi. Ni katika kuhakikisha kuwa ikishambuliwa nchi moja ya Ulaya nchi zote zitasaidia .

Kupewa tena sila kwa Ujerumani , Ufaransa ilishindwa kuzuwia. Kwani umoja wa Ulaya pia unajumuisha Ujerumani ambayo pia imepewa mwaliko kujiunga na NATO hapo May 1955. Ujerumani ikaanza kujiamini na ikaanzisha na jeshi lake Bundeswehr .