1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wapigania makubaliano ya nyukilia

Isaac Gamba
8 Novemba 2017

 Wabunge wa Marekani  wameonesha wazi  kwamba wanapanga kuhakikisha  Marekani inatekeleza makubaliano ya nyukilia ya mwaka 2015 yaliyofikiwa kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani.

https://p.dw.com/p/2nFNf
Luxemburg Treffen der EU-Außenminister PK Federica Mogherin
Picha: Getty Images/AFP/J. Thys

 Hayo yamebainishwa na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federeca Moghereni aliyeko ziarani nchini Marekani katika kikao chake na waandishi wa habari hapo jana.

Huku akisisitiza kuwa Umoja wa Ulaya hauna mpango wa kuingilia siasa za ndani za Marekani lakini aliwasilisha ujumbe kuwa Umoja wa Ulaya unapinga sheria yoyote mpya itakayo changia kuvunja makubaliano hayo.

Mnamo Oktoba 13, Trump  alitoa kauli iliyoashiria kuyatia doa makubaliano hayo baada ya kukataa kuthibitisha kuwa Iran ilikuwa  inatekeleza makubaliano hayo licha ya wakaguzi wa kimataifa kusema kuwa ilikuwa inatekeleza kama inavyopasa.

Chini ya makubaliano hayo Iran ilikubali kupunguza mipango yake inayohusiana na silaha za nyukilia huku pia ikipaswa kuondolewa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi yake.

 

Trump aweka mashakani majaliwa ya makubaliano ya nyukilia

US-Präsident Donald Trump hält seine Rede in der Nationalversammlung in SeoulSüdkorea, US-Präsident Donald Trump hält seine Rede in der Nationalversammlung in Seoul
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Reuters/L.Jin-man

Umuzi huo wa Trump umeweka mashakani mustakabali wa makubaliano hayo ya nyukilia yaliyofikiwa kati ya Iran na Umoja wa Ulaya  pamoja na mataifa sita yenye nguvu ambayo ni Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Marekani.

Bunge la Marekani lina muda  hadi katikati ya mwezi wa desemba wa kuamua  kurejesha vikwazo  vilivyoondolewa chini ya makubaliano hayo ya nyukilia suala  ambalo wanadiplomasia wachache wanalitarajia.

Moghereni alijaribu kujizuia kujiingiza moja kwa moja katika mjadala unaohusu suala hilo katika bunge la Marekani licha ya kusisitiza juu ya nia yake ya kutaka Marekani isalie katika makubaliano hayo.

Mkuu huyo wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya  amesema tayari ameshaweka wazi juu ya utayarifu wake katika kusaidia kuona wabunge wa Marekani wanapata suluhisho litakaloianya Marekani ibakie katika makubaliano hayo ya nyukilia.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi  Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki Yukia Amano  aliwaeleza waandishi wa habari kuwa  itakuwa  jambo baya zaidi iwapo Iran itasitisha kutekeleza itifaki  ya ziada ya makubaliano hayo inayoitaka itoe taarifa muhimu zinazohitajika zitakazolisaidia shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki (IAEA) kuweza kuthibitisha  iwapo nchi hiyo inatekeleza ipasavyo  makubaliano hayo ya nyukilia. Chini ya makubaliano hayo ya mwaka 2015 Iran ilikubali kutekeleza .

Akizungumza na waandishi wa habari Amano amesema kuwa katika ziara yake nchini Iran  mwezi uliopita  maafisa wa Iran walimhakikisia kuwa wataendelea kutekeleza makubaliano ya nyukilia na kuwa hawatakuwa wakwanza kujitenga na makubaliano hayo.

A lipoulizwa iwapo Iran imemuonesha dalili zozote kuwa inaweza kujitenga na kutotekeleza masharti hayo ya ziada Amano alijibu kuwa Iran haisemi nini kitatokea lakini kwa mtazamo wake  lolote linaweza kutokea.

Mwandishi: Isaac Gamba/afpe/rtre

Mhariri:Hamidou Oummilkheir