1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya watishia kususia mkutano na Marekani

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbLL

BALI

Wakati mazungumzo yanayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa yakiingia hatua yake ya mwisho mataifa ya Ulaya leo yametishia kususia mkutano wa hali ya hewa unaongozwa na Marekani mwezi ujao venginevyo serikali ya Marekani inakubali makubaliano yenye kutaja viwango vya tarakimu kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi zenye kuongeza hali ya ujoto duniani.

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba wakati unayoyoma kufikia makubaliano yenye lengo la kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba utakaochukuwa nafasi ya Itifaki ya Kyoto na kwamba mazungumzo ya Bali yako hatarini kusambaratika.

Waziri wa mazingira wa Ujerumani ambaye anahudhuria mkutano huo wa Bali nchini Indonesia leo ameshutumu kukosekana kwa ushujaa kwa Marekani na nchi zinazoinukia kiuchumi katika kufikia muafaka wa mazungumzo hayo.

(O-TON Gabriel)

Marekani,Japani,Urusi na serikali nyengine kadhaa zimegoma kukubali lugha iliomo kwenye rasimu ya waraka wa makubaliano inayodokeza kwamba mataifa tajiri yenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani yafikirie kupunguza utowaji wa gesi zenye kuathiri mazingira kwa asilimia 25 hadi asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kwa hoja kwamba viwango mahsusi vitawekea kikomo ugwe wa mazungumzo ya kipindi cha usoni.