1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waunga mkono mchakato wa demokrasia

Martin,Prema5 Februari 2011

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amehakikisha kuwa mchakato wa demokrasia nchini Misri utaungwa mkono na Ujerumani na Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/QyVQ
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) spricht am Samstag (05.02.11) in Muenchen bei der 47. Muenchner Sicherheitskonferenz im Hotel Bayerischer Hof. Die Muenchner Sicherheitskonferenz findet von Freitag (04.02.11) bis Sonntag (06.02.11) im Hotel Bayerischen Hof in Muenchen statt. (zu dapd-Text) Foto: Oliver Lang/dapd
Kansela wa Ujerumani, Angela MerkelPicha: dapd

Merkel, alitamka hayo alipohotubia mkutano wa usalama wa kimataifa mjini Munich, kusini mwa Ujerumani. Amesema umma wa Misri unaungwa mkono na ameonya kutochukuliwa hatua za haraka. Akaongezea kuwa utaratibu wa kidemokrasia unapaswa kufanyika kwa amani na busara.

Merkel alisema kuwa Umoja wa Ulaya, hapo jana kwa pamoja, uliamua kuwa unataka ushirikiano mpya ili kusaidia kuleta mageuzi hayo kama majirani wao katika mwambao wa Afrika ya Kaskazini.

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton alipozungumza kwenye mkutano huo mjini Munich, alitoa mwito wa kufanyika mageuzi halisi ya demokrasia katika kanda hiyo, kufuatia machafuko ya nchini Misri.