1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamke 1 hufariki kila baada ya dakika 2 kwa ujauzito

23 Februari 2023

Umoja wa Mataifa umesema katika kila baada ya dakika mbili, mwanamke mmoja hufariki dunia kutokana na ujauzito au matatizo ya kujifungua. Hii ni licha ya viwango vya vifo vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi kupungua.

https://p.dw.com/p/4Nrxc
Symbolbild I Schwangerschaft in Indien
Picha: Donatella Giagnori/MAXPPP/Eidon/picture alliance

Umoja wa Mataifa umesema katika kila baada ya dakika mbili, mwanamke mmoja hufariki dunia kutokana na ujauzito au matatizo ya kujifungua.

Hii ni licha ya viwango vya vifo vinavyosababishwa na matatizo ya uzazi kupungua kwa theluthi moja katika miaka 20 iliyopita.

Umoja wa Mataifa umesema viwango hivyo vilipungua pakubwa kati ya mwaka 2000 na 2015. Lakini vilisimama kwa kiasi kikubwa kati ya mwaka 2016 na 2020. Katika mataifa mengine hali ilidorora na kurudi nyuma.Utoaji mimba usio salama Tanzania

Kwa jumla viwango vya vifo vya kina mama vilipungua kwa asilimia 34.3 katika kipindi cha miaka 20 kutoka vifo 339 kati ya wajawazito 100,000 mnamo mwaka 2,000 hadi vifo 223 katika mwaka 2020.

Takwimu hizo ni kulingana na ripoti ya shirika la Afya DUniani WHO na mashirika mengine ya Umoja wa Ulaya.