1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yatiwa moyo na makubaliano ya Iran

18 Mei 2010

Umoja wa Mataifa umeyaelezea makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran, Brazil na Uturuki, katika kupunguza hali tete na ya wasi wasi kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran, kuwa ni ya kutia moyo

https://p.dw.com/p/NQVg
Nembo ya UN

Iran hata hivyo imesema makubaliano hayo ni lazima yaendane na sheria na taratibu za umoja huo.

Ali Akbar Salehi
Mpatanishi wa Iran katika mzozo wa nyuklia Ali Akbar SalehiPicha: ISNA

Mpatanishi mkuu wa Iran katika mzozo wa nyuklia, Ali Akbar Salehi, amesema makubaliano hayo yanaonesha Iran iko tayari kwa mashauriano.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaitaka Iran kusitisha urutubishaji wa madini ya uranium.Katika makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Brazil pamoja na Uturuki, Iran imekubali kurutubisha nje ya nchi madini hayo ya uranium, ambapo Uturuki itaipatia akiasi cha madini hayo kwa ajili ya utafiti wa madawa.

Lakini kwa upande wake Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Hermann van Rompuy amesema jumuiya ya kimataifa bado ina shaka na mpango huo wa nyuklia wa Iran.

Ujerumani, Uingereza na Ufaransa nazo zimelezea wasi wasi baada ya Iran kusema kuwa itaendelea kurutubisha madini ya uranium pamoja na kufikiwa kwa makubalino hayo ya hapo jana.

Mwandishi:Aboubakary Liongo