1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Unaweza kuzuia njaa Afrika?

Abdu Said Mtullya28 Machi 2013

Jee Afrika itaweza kuondokana na njaa? Mahitaji ya chakula yanazidi kuwa makubwa nchini India na China. Lakini barani Afrika, mara kwa mara linatokea baa la njaa.

https://p.dw.com/p/184cS
A Somali woman from southern Somalia and her children prepare leafy vegetables to cook at a refugee camp in Mogadishu, Somalia, Tuesday, Aug 9, 2011. The number of people fleeing famine-hit areas of Somalia is likely to rise dramatically and could overwhelm international aid efforts in the Horn of Africa, a U.N. aid official said Tuesday. (ddp images/AP Photo/Farah Abdi Warsameh)
Welthungerhilfe Horn von Afrika SomaliaPicha: AP

Hata hivyo bara hilo linaweza kuondokana na njaa. Ila dhamira ya kisiasa inakosekana. Dhamira ya kisiasa kwa ajili ya kuendeleza kilimo barani Afrika ndio haipo. Lakini pana habari njema: Serikali za Afrikam wafadhili na Umoja wa Mataifa wameigundua tena sekta ya kilimo barani Afrika.

Kwa pande hizo zote, sera ya maendeleo ya viwanda chini ya uongozi wa serikali ilizingatiwa kama dini kwa kipindi cha karibu miaka 20. Lakini ardhi ilikuwa ile ile ya jana.

Lakini viongozi wa Afrika walifungukuka macho kufuatia vurumai za malighafi,zilizoandamana na mfumuko wa bei za vyakula mnamo mwaka wa 2008 uliochangia katika kusababisha njaa.

Matokeo yake ni kwamba nchini Ujerumani pia kwenye wizara ya maendeleo mada juu ya mkakati wa maendeleo ya kilimo inaandaliwa tena-yaani sera ya maendeleo inayowafiki na hali halisi ya barani Afrika.Hadi leo watu zaidi ya 900,000,000 yaani asilimia 90 bado wanayakidhi mahitaji yao ya maisha kwa kutegemea kilimo.

TO GO WITH AFP STORY BY AARON MAASHO 'ETHIOPIA-DROUGHT-UN' --- Anero Argo sprinkles fertilizer in a recently seeded bean field near the town of Boricha, in southern Ethiopia, on August 30, 2008. Ethiopia suffered severe floods last year which destroyed most of the food crop. This year a drought has worsened the situation and food prices have soared 330 percent. Lack of rain in the main February to April wet season in Ethiopia has left at least 75,000 Ethiopian children under five at risk from malnutrition, accoring to the UN's Office for the Coordination of Humanitarian Affairs (OCHA) and some eight million people in need urgent food relief. The top UN aid official John Holmes on September 1, 2008 called for greater international efforts to help millions of Ethiopians suffering from a severe drought. AFP PHOTO/Roberto SCHMIDT (Photo credit should read ROBERTO SCHMIDT/AFP/Getty Images)
Kilimo nchini EthiopiaPicha: AFP/Getty Images

Japo ni vigumu kufananisha: jaribu kumfikiria mtu anaekuja na mawazo ya ajabu ya kuviondoa viwanda vya kazi za mikono , vidogo vidogo na vya kati nchini Ujerumani - viwanda vinavyotoa milioni ya nafasi za ajira na vinavyojenga sehemu ya msingi wa uchumi wa nchi.

Swali la mradi wa ripoti za DW"Jee Afrika itaweza kuondoa njaa" lina shabaha mbili-Jee itaweza kuondoa njaa nyumbani na kukidhi mahitaji ya malighafi kwa ajili ya uchumi wa nchi kama China, India na nyinginezo-mahitaji yanayozidi kuongezeka.

Kwa usemi mwingine, jee bara la Afrika litaweza kuyakidhi mahitaji yake ya chakula katika kipindi cha muda mfupi na kuweza kuuza chakula nje ya bara hilo?

Utafiti katika Afrika Mashiriki na Magharibi na katika maabara za Ujerumani umetoa jibu lifuatalo: ndiyo itawezekena, ikiwa viongozi n wafadhili watadhamiria.

Hakuna motisha wa vitega uchumi

Na hapa ndipo panapoanzia habari mbaya. katika nchi nyingi za Afrika dhima kwa wakulima inatimizwa kwa kauli tu. Kote, yanakosekana yale ambayo katika hati nyingi juu ya kile kinachoitwa sera ya uwezeshaji-yaani msingi wa kuwawezesha wakulima kuondokana na kilimo cha kijungujiko na hivyo kuzalisha ziada.

Mfano ni Ethiopia; asilimia 85 ya watu 90,000,000 wa nchi hiyoa wanakidhi maisha yao kutokana na shughuli za kilimo. Lakini serikali, kana kwamba inataka kukumbuka enzi za usoshalisti inawakataza wakulima kumiliki ardhi.Hata ardhi ya kukodisha haina uhakika.

Kutokana na hayo wakulima wanakosa ari ya kuekeza katika vipande vidogo vidogo vya ardhi, kana kwamba ni wajibu wao kuilinda ardhi na hatari ya kumomonyoka. Badala yake wananasa katika mtego wa madeni kutokana na kukubali mbegu na dawa ghali zinazoibabua ardhi.Ikiwa mavuno ni hafifu madeni yanaongezeka.

Mpaka leo bado mafalahi wengi hawapati fursa za mikopo ya benki ili kuweza kununua vifaa vya kisasa na hivyo kuweza kuongeza tija.

Tatizo jingine kwa wakulima wengi ni kushindwa kupata masoko kwa mazao yao mpaka katika karne hii.

Aghalabu barabara hazipitiki wakati wa masika.

Uchunguzi umeonyesha kwamba asilimia 50 ya samaki wanaozea njiani kabla ya kufikishwa sokoni.Hicho kwa hakika ni kiwango kikubwa. Orodha ya kosoro ni ndefu.

Bila ya kilimo havitajengwa viwanda barani Afrika:

Yanayohitajika ni machache ili kuweza kuongeza tija na hivyo kuinua kiwango cha mavuno ya wakulima.

Hapa inapasa ieleweke vizuri. Lengo siyo kuendeleza viwanda na kukipuuza kilimo.Sekta zote ni muhimu:kupanga ni kuchagua!

Ardhi bora na mashine.

Mchakato wa kujenga viwanda unapaswa kosonga mbele kwa nguvu barani Afrika ili kakao iweze kushuhgulikiwa mjini Abidjan badala ya mjini Hamburg.

Serikali za Afrika na wafadhili pia wanapaswa kusimama katika safu ya usawa katika ushirikiano wa uzalishaji wa chakula.

Nafasi ni nzuri. Baada ya harakati za watu wa a Tunisia za mwaka wa 2011 zilizowafagilia mbali wanasiasa

-harakati zilizoleta upepo wa mabadiliko kaskazini mwa Afrika hadia katika za kiarabu, Afrika inapswa kuchukua tahadhari.

Mwenye njaa hana subira.Njaa inaweza kuwa silaha ya kisiasa.

Wanasiasa wa Ulaya wanaweza kuziona kambi za wakimbizi katika Lampedusa na Malta zinazoonyesha ni kwa kiasi gani njaa inaweza kusababisha hali ya mtamauko. Wakati sasa umeiva wa kufikia ruwaza mpya ya kilimo cha Afrika.

Mwandishi: Schadomsky ,Ludger
Tafsiri: Mtullya Abdu.
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman