1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Unyanyasaji wa raia wa kisomali nchini Kenya

23 Januari 2013

Wanaharakati wa haki za binaadamu nchini Kenya wanasema raia wa Somalia wanakabiliwa na mashambulizi kutoka makundi fulani ya watu na kutoka kwa polisi tangu serikali itoe amri ya kuwataka wakimbizi warejee makambini.

https://p.dw.com/p/17QGm
Raia wa kisomali eneo la Eastliegh,Nairobi
Raia wa kisomali eneo la Eastliegh,NairobiPicha: Bettina Rühl

Itakumbukwa mwaka 2011, kutokana na waasi wa Somalia al Shabaab wenye mfungamano na al-Qaeda kufanya mashambulizi na utekeaji nyara katika maeneo ya mpakani, jeshi la Kenya liliingia katika ardhi ya Somalia kukabiliana na kundi hilo. Hivi punde Sudi Mnette alizungumza na Kamishna wa Haki za Binaadamu wa Kenya aliyemaliza muda wake, Samuel Tororei. Kwanza alitaka kujua anafahamu nini kuhusu vitendo hivyo vya ukiukwaji wa haki za binadamu? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Josephat Charo