1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Unyanyasaji wakithiri katika magereza Nchini Mynmar

9 Septemba 2016

Taarifa zinasema kuwa maelfu ya wafungwa katika kambi za vituo vya kazi kwa wafungwa nchini Myanmar wanateswa , kupigwa na kutumikishwa kazi ngumu pamoja na vitendo vingi vya ukiukwaji kwa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/1Jz4F
Waandamaji katika gari la polisi wakionyesha mikono nchini MyanmarPicha: picture-alliance/dpa/N. Chan Naing

Vitendo hivyo vinaibuliwa na uchunguzi ambao unaendelea kwa miezi kadhaa sasa tangu Aung San Suu Kyi kutoka chama cha National League for democracy NLD aingie madarakani mwezi March ambako katika vituo hivyo wafungwa hulazimishwa kufanya kazi za kilimo katika mashamba yaliyo chini ya kitengo cha kurekebisha tabia za wafungwa ama katika mashamba binafsi ya watu

Maelfu ya wafungwa na maafisa wa zamani wa magereza waliofanyiwa mahojiano wanasema kitendo hicho kinawatengenezea picha ya mazingira magumu zaidi yaliyoambatana na rushwa kutoka kwa walinzi wa magereza ambao huwalazimisha wafungwa hao kutoa rushwa ikiwa wanataka kuepuka vipigo na adhabu na kazi ngumu

Kwa mujibu wa uchunguzi Magereza kupata faida kubwa kutokana na kuuza vifaa ambavyo ni mazao ya kazi ngumu wanazolazimishwa wafungwa kufanya ikiwa ni kinyume na na mkataba wa kupinga utumikishwaji uliosainiwa na nchi hiyo madai amabayo hata hivyo hayakuthibitishwa baada ya waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo kukataa kuongea chochote kuhusiana na suala hilo

Myanmar Aung San Suu Kyi
Mwenyekiti wa chama cha NLD Aung San Suu KyiPicha: Getty Images/AFP/Ye Aung Thu

Ziyar Lin mwenye umri wa miaka 25 aliwahi kuwa afisa wa polisi na baadaye kufungwa kwa miaka miwili na kupelekwa kituoni hapo kwa kosa la kupigana na kiongozi wake akiwa anasema akiwa njiani kuelekea kituoni hapo askari walimfunga pingu na akiwa huko alikuwa akipata vipigo mara kwa mara na kazi ngumu anasema

"Nilishutumiwa kuwa nafanya kazi taratibu kwa hiyo nilipigwa sana mgongoni na kila siku nilichwapwa angalau viboko 30"

Lakini baada ya mwezi mmoja mama yake alitoa pesa kwa kiongozi wa gereza ili kuzuia asiendelee kupingwa baada ya hapo akaanza kupewa kazi rahisi kama vile kuchemsha maji na kuandaa kahawa kwa ajili ya maafisa wa magereza kazi ambayo alifanya mpaka siku alioachiwa huru wafungwa masikini kwa upande wao, wao hawana njia nyingine zaidi aidha kutoa rushwa ya ngono au kufanya kitu kingine chochote kinachoweza kuthaminishwa ili kuepuka kazi ngumu

Mfumo wa kazi gerezani unatoa mwanya wa rushwa

Khim Maug afisa wa zamani wa magereza anasema mfumo wa ufanyaji kazi katika magereza unatoa nafasi kwa mianya ya rushwa kwa sababu inampa mamlaka kamili kiongozi wa cheo kama chake kugawa kazi na kuamua ni adhabu gani anafaa kutolewa

Piyamal Pichaiwongse naibu wa masuala ya mahusiano wa shirika la kazi duniani ILO nchini Myanmar, anasema makubaliano yoyote ya kuwaweka wafungwa katika hatarini kwa kufanya kazi na makampuni ni kuvunja sheria ya mwaka 1930 ya kukomesha ajira za lazima ambayo pia ilitiwa saini na nchi hiyo pamoja na kuwa yeye pia hakuweza kuzungumza kuhusu madai hayo kwa kuwa kumekuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuthibitisha.

Nae naibu mkurugenzi wa kitengo cha kurekebisha tabia za wafungwa Min Tun Soe anasema utumikishwaji na kazi ngumu ni mambo ambayo yalikuwa yanafanika zamani na kuwa kulifanyika mabadiliko chini ya rais aliyepita Thein Sen mwaka 2011 na 2015 ambayo imesaidia kuboresha hali za wafungwa

Mwandishi: Celina Mwakabwale/Reuters

Mhariri:Yusuf Saumu