1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upekuzi wakati wa mkutano wa G8 ulikuwa kinyume na sheria.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkPs

Karlruhe, Ujerumani.

Mahakama kuu ya shirikisho nchini Ujerumani imeamua kuwa msako uliofanywa dhidi ya wapinzani wa mkutano wa mataifa tajiri duniani G8 uliofanyika katika mji wa Heiligendamm, nchini Ujerumani May mwaka jana ulikuwa kinyume na sheria. Mahakama hiyo imesema kuwa wanaharakati waliokuwa wanapinga mkutano huo wa G8 hawakujikusanya kuunda kundi la kigaidi na kwa hiyo msako hakuwa katika misingi ya kisheria chini ya ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa shirikisho la Ujerumani. Polisi wa Ujerumani , wakati huo , wakifanya upekuzi katika nyumba 40 katika majimbo sita, na kukamata kompyuta na nyaraka kadha. Wapinzani wa mkutano wa G8 walituhumiwa kuhusika na mashambulizi kadha ya mabomu ya moto katika wakati kuelekea mkutano huo. Mahakama hiyo imetoa hukumu kuwa majimbo binafsi na sio serikali ya shirikisho yalikuwa yanadhamana ya kuwafuatilia watuhumiwa wa uhalifu.