1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upigaji kura wamalizika Cambodia

27 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EkgQ

PHNOM PENH CAMBODIA

Wananchi wa Cambodia wamekamilisha shughuli ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika hii leo.

Waziri mkuu Hun Sen anatarajiwa kurudi tena madarakani kuongoza kipindi kingine cha miaka mitano baada ya kuongoza nchi hiyo miaka 23.

Kampeini za uchaguzi ziligubikwa zaidi na suala la mvutano wa mpaka na Thailand na kumfaidisha zaidi waziri mkuu huyo Hun Sen na chama chake cha Cambodia Peoples Party CPP.

Chama cha CPP kimetawala nchini humo tangu nchi hiyo kuanzisha mfumo wa demokrasia mwaka 1993.Mpinzani mkuu katika uchaguzi huo miongoni mwa vyama 11 vilivyogombea ni chma cha Sam Rainsy.Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa baadae wiki ijayo.