1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

USA Muslime 11.9.

Sekione Kitojo8 Septemba 2010

Siku chache kabla ya kumbukumbu ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani, inaonekana kuna wimbi la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

https://p.dw.com/p/P77h
Haya ni baadhi ya matukio yanayoonyesha upinzani dhidi ya Uislamu nchini Marekani. Waandamanaji wakipinga ujenzi wa kituo cha Kiislamu.Picha: AP

Siku chache kabla ya kumbukumbu ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani , inaonekana kuna wimbi la chuki dhidi ya Uislamu nchini humo. Tukio lililopangwa la kuchoma kitabu cha Koran pamoja na upinzani dhidi ya ujenzi wa kituo cha Kiislamu mjini New York , ni masuala yanayoleta hali ya wasi wasi , lakini hakuna sababu ya kuyachukulia masuala hayo kwa jazba.

Je Marekani ni adui wa Uislamu ? Swali hili hivi sasa haliwashughulishi tu watu nchini Marekani , lakini ni duniani kote. Tukio lililopangwa la kuchoma nakala za kitabu kitakatifu kwa Waislamu cha Koran tayari limekwisha chukuliwa na baadhi ya nchi za Kiislamu kuwa Marekani ni adui wa Uislamu. Hofu ya kutokuwa na uvumilivu wa kidini katika nchi ambayo inajinasibu na uhuru wa kidini , ni kama doa jeusi katika kumbukumbu ya kila mwaka ya mauaji ya kinyama ya shambulio la Septemba 11, yaliyotokea mwaka 2001.

Kitu gani kimetokea tangu wakati huo nchini Marekani ? Je nchi hii imetafakari vya kutosha kuwa na mahusiano na Waislamu, na kubadilisha msimamo wa msimamo mkali. Je nchi hii imesahau njia yake yenye mafanikio ya kuwajumuisha watu wote katika nchi hiyo? Hivi karibuni kumekuwa na upinzani dhidi ya mipango ya ujenzi wa kituo cha Kiislamu karibu na eneo lililotokea shambulio la kigaidi la Septemba 11 mjini New York.Wawakilishi wa Kiislamu, Wakristo na Wayahudi walitoa mapendekezo ya uvumilivu na walizungumzia dhidi ya kuongezeka kwa wimbi la hofu na kutokuvumiliana.

Wawakilishi wa ngazi ya juu wa serikali , kama waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton , ameeleza na kutoa shutuma kali dhidi ya mpango huo wa kuchoma nakala za kitabu cha Koran. Hali hii isiyopendeza , haina sababu ya msingi ya kuonyesha jazba. Watu wenye imani kali ya kidini wapo nchini Marekani.

Mwanzoni mwa karne ya 19 kulikuwa na hali ya upinzani dhidi ya Wakatoliki, ambao hivi leo ni sehemu ya jamii ya Wamarekani . Katika karne ya 20 na hadi sasa, wanaharakati wa kutetea haki za wanawake wanaotoa mimba wamekuwa wakipambana na Wakristo wenye imani kali.

Pamoja na hayo kuna njama dhidi ya mataifa ya magharibi licha ya kuwa nchini Marekani kuna nguvu za kuufanya Uislamu kuwa katika hali sawa katika jamii.

Vita viwili vinavyoendeshwa na Marekani katika mataifa ya Kiislamu , bila shaka vimeiweka hali ya Waislamu nchini Marekani katika hali ngumu, na kuna matatizo unapoangalia vile Marekani inavyoelekea katika kupambana na Uislamu. Katika hotuba yake maarufu mjini Cairo, rais Barack Obama aliuthamini Uislamu na Waislamu kote duniani aliwanyooshea mkono. Idadi ya matukio ya kutumia nguvu yenye hamasa za kidini nchini Marekani imepungua. Makundi kadha ya waumini wa Kiislamu nchini Marekani wanataka kutumia mwisho wa mfungo wa Ramadhan , katika mwaka huu kusherehekea kwa kuwakumbuka kwa pamoja wahanga wa shambulio la Septemba 11. Maana ya Uislamu ni amani , amesema rais wa zamani wa Marekani George W. Bush katika msikiti mmoja mara baada ya shambulio la kigaidi.

Mwandishi : Daniel Scheschkewitz / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Abdul-Rahman