1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Kenya wataka Raila atangazwe Rais

11 Agosti 2017

Upinzani Kenya unaamini mgombea wake Raila Odinga ameshinda urais, ukikataa matokeo yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Uchaguzi IEBC yanayomuonesha Rais Uhuru Kenyatta akiongoza katika uchaguzi uliokuwa na mashaka.

https://p.dw.com/p/2i38X
Raila Odinga
Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Curtis

Awali waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, anayeongoza timu ya waangalizi wa uchaguzi katika kituo cha Carter, alisema ana imani na mfumo wa kielektroniki uliotumika katika uchaguzi wa Kenya. Zaidi ya waangalizi 400 wa kimataifa walishuhudia uchaguzi huo wa Jumanne iliyopita.

Kura zinaendelea kuhasebiwa na matokeo kutolewa na IEBC
Kura zinaendelea kuhasebiwa na matokeo kutolewa na IEBCPicha: Getty Images/AFP/L. Tato

Hata hivyo upinzani unaedelea kudai kwamba uhesabuji wa kura ulikuwa wa udanganyifu baada ya Odinga kusema Jumatano kwamba mtambo wa kielektroniki wa kupigia kura ulidukuliwa na matokeo yalifanyiwa ukarabati. Tume ya IEBC inaendelea kusisitiza kwamba mtambo wake wa kielektroniki wa kupiga kura haujaathiriwa, licha ya majaribio dhahiri ya kutaka kufanya hivyo.