1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Upinzani nchini Poland wafanya mkutano mkubwa wa kampeni

1 Oktoba 2023

Mamia kwa maelfu ya watu nchini Poland wamehudhuria leo mkutano mkubwa wa kampeni wa upande wa upinzani ikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kuwa wa ushindani mkali.

https://p.dw.com/p/4X1Kl
Mkutano wa upinzani, Poland
Upinzani unasema watu milioni 1 wamehudhuria mkutano mjini WarsawPicha: Slawomir Kaminski/Agencja Wyborcza.pl via REUTERS

Akihutubia mkutano huo uliofanyika kwenye viunga vya mji mkuu, Warsaw, kiongozi wa chama cha upinzani cha  Civic Platform (PO) Donald Tusk ameuambia umma uliokusanyika kuwa "mabadiliko makubwa yanakuja na ni ishara ya Poland kuzaliwa tena"

Inakadiriwa watu takribani milioni 1 wamehudhuria mkusanyiko huo kuelekea uchaguzi wa mnamo Octoba 15 ambao upinzani unasema utaamua juu ya hatma ya demokrasia ya Poland na nafasi ya nch hiyo ndani ya Umoja wa Ulaya.

Kura za maoni ya umma zinabashiri ushindi kwa chama tawala cha Law and Justice (PiS) lakini huenda kitashindwa kupata viti vya kutosha kuunda serikali kutokana na hasira ya wapiga kura juu ya kupanda kwa gharama za maisha na kuanguka kwa misingi ya kidemokrasia.