1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Upinzani Venezuela wamsajili mgombea wa uchaguzi wa rais

Bruce Amani
27 Machi 2024

Muungano mkuu wa upinzani nchini Venezuela umesema umefanikiwa kumsajili mgombea atakayepambana na dhidi ya Rais Nicolas Maduro katika uchaguzi wa nchi hiyo wa mwezi Julai -- lakini sio yule waliyemtaka.

https://p.dw.com/p/4e9nv
Kiongozi wa upinzani Venezuela Maria Corina Machado
Kiongozi maarufu wa upinzani Maria Corina Machado alifungiwa kushikilia wadhifa wa umma Picha: Pedro Rances Mattey/Anadolu/picture alliance

Huku kiongozi maarufu Maria Corina Machado akliwa amezuiwa kushikilia wadhifa wa umma, mpango wao ulikuwa ni kumsajili mgombea mwingine mbadala, profesa wa Chuo Kikuu Corina Yoris mwenye umri wa miaka 80.

Lakini muungano huo ulijikuta umezuiwa kufanya hivyo kabla ya muda wa mwisho uliowekwa wa Jumatatu usiku wa manane. Baraza la Kitaifa la Uchaguzi - CNE limetoa jina la kushangaza la Edmundo Gonzalez Urruti, mtalaamu wa siasa na balozi wa zamani, kuwa mgombea wa Jukwaa la Umoja wa Kidemokrasia - PUD. Uchaguzi wa Venezuela unapangwa mwezi Julai

Muungano huo umesema katika taarifa kuwa chaguo hilo la mgombea wao ni la muda ikizingatiwa ugumu wa kumsajili mgombea aliyechaguliwa hadi sasa.

Soma pia: Venezuela wapiga kura kumchaguwa mpinzani wa Maduro

Maduro mwenye umri wa miaka 61 anatafuta kurefusha muda wake wa muongo mmoja madarakani kwa kupata muhula wa tatu wa miaka sita, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu kuanguka kwake katika utawala wa kibabe na kuukandamiza upinzani.