1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani waitisha maandamano makubwa nchini Georgia

6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Ckw0

Upinzani nchini Georgia umewataka wafuasi wake wajitokeze kwa wingi kufanya maandamano katika barabara za mji mkuu Tbilisi hii leo.

Mwito huo umetolewa baada ya rais wa Georgia, Mikhail Saakashvili kushinda awamu ya kwanza ya uchaguzi wa rais.

Matokeo ya kwanza ya uchaguzi huo yalimpa ushindi rais Saakashvili wa asilimia 53.8 dhidi ya wapinzani wake. Rais Saakashvili amewaambia wafuasi wake katika makao makuu ya kampeni zake mjini Tbilisi kwamba uchaguzi uliofanyika ni ushindi wa nchi nzima ya Georgia, lakini wapinzani wake wanadai kwambwa uchaguzi huo ulikumbwa na mizengwe.

Mpinzani mkuu wa rais Saakashvili, Levan Gechechiladze ametangaza ameshinda uchaguzi huo akisema kumekuwa na udanganyifu katika zoezi la kuhesabu kura.