1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uranium yatishia usalama Arusha

9 Novemba 2012

Ripoti zilizotokeza hivi karibuni kupitia vyombo kadhaa vya habari barani Afrika zinaeleza kwamba wakulima mkoani Arusha, Tanzania wanatumia vumbi la uranium kulinda mazao yao dhidi ya magonjwa ya mimea na wadudu.

https://p.dw.com/p/16fxX
A farmer prepares water channels in his maize field in Ngiresi near the Tanzanian town of Arusha on Tuesday, July 17, 2007. Millions of farmers around the world will be affected by a growing movement to change one of the biggest forces shaping the complex global food market: subsidies. Many experts agree farmers need help to grow food year in and year out, but Western farmers may get too much and African farmers too little. (AP Photo/Karel Prinsloo)
Kilimo barani AfrikaPicha: AP

Taarifa hizo zimethibitishwa na kamisheni ya nishati ya Atomiki nchini humo yenye makao yake makuu mjini Arusha.Kamisheni hiyo tayari imeuonya umma kwa jumla na hasa wakulima juu ya kutumia vibaya kemikali hiyo hatari.

Kamisheni hiyo imefahamisha kwamba hatua hiyo inahatarisha sio tu maisha ya wakulima bali hata pia umma kwa jumla. Mamilioni ya watu wanaotumia chakula cha mahindi maharagwe na nafaka nyinginezo zilizohifadhiwa kwa njia ya kutumia kemikali hizo wako katika kitisho kikubwa cha kupata maradhi ya saratani na maradhi mengine.

Shirika la Atomiki lazungumzia suala hilo

Mkurugenzi wa shirika hilo la Atomiki Tanzania Prof Iddi Mkilaha akizungumzia suala hilo amesema kuna baadhi ya wafanyibiashara walaghai wanaoagiza Uraninium kutoka nchi kadhaa jirani na kuuza kamekali hiyo kwa wakulima na kuwadanganya kwamba vumbi la madini hayo ndio njia pekee ya kupambana na wadudu wa mimea na matatizo mengine katika mimea kwa jumla. Hata hivyo taarifa hizi zimezusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa watu akizungumza na Dw kwa njia ya simu hivi punde msemaji wa wizara ya maendeleo ya kigeni kuhusu sera ya Ujerumani ambaye pia ameandika barua ya wazi kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi nishati ya Atomiki duniani IAEA,na ambaye amewahi kutembelea maeneo ya miradi ya Uranium Tanzania kuhusu suala hilo,Ute Koczy amesema "Kinachoendelea Tanzania ,wanaohusika na kadhia hii ,chanzo chake na wanaopigia debe kadhia hii hawajawekwa wazi lakini cha muhimu na msingi ni kwamba ipo haja kubwa kwa serikali ya Tanzania na mashirika husika kuulinda umma na kuutahadharisha.''

Workers hoeing field, Kabale, Uganda, Africa
Kilimo cha jembe la mkono AfrikaPicha: picture alliance/David Poole/Robert Harding

Bibi Koczy ambaye ni mbunge wa Ujerumani ameandika pia barua ya wazi juu ya suala hilo kwa rais na waziri mkuu wa Tanzania. Kwa upande wake Prof Mkilaha mkurugenzi mkuu wa TAEC amefahamisha kwamba tayari shirika hilo limefanikiwa kuwatambua baadhi ya wafanyibiashara wanaohusika na kadhi hii na limeshirikiana na polisi kuwakamata.Mtaalamu wa Nuklia katika shirika hilo Dr Mwijarubi akitoa ufafanuzi kuhusu madhara ya kemikali hii amesema pindi mtu anapovuta hewa ya vumbi hilo la madini ya Uranium linaingia moja kwa moja kwenye mapafu na kusababisha saratani ya mapafu na viuongo vingine mwilini. Halikadhalika kwa mujibu wa wataalamu nafaka zilizoingia madini hayo huenda zikasababisha madhara makubwa sio tu kwa wakulima wahusika bali pia kwa wale wakulima wanaosagisha kwenye mitambo ambako imetokea nafaka aina hiyo zimesagishwa.

Ute Koczy, Entwicklungspolitische Sprecherin Bündnis 90/Die Grünen Foto: Stephan Röhl/Heimrich-Böll-Stiftung 25.11.2010 Quelle: http://www.flickr.com/photos/boellstiftung/5223665150/in/photostream/ Lizenz: creative commons: Namensnennung - Weitergabe unter gleichen Bedingungen 2.0 US-amerikanisch (nicht portiert) (CC BY-SA 2.0)
Mbunge wa Ujerumani Ute KoczyPicha: Stephan Röhl/Heimrich-Böll-Stiftung

Katika suala hilo Sudi Mnette amezungumza na Julius Nimbu Mkurugenzi wa Mazingira ofisi ya makamu wa rais wa Tanzania. Kusikiliza mahojiano hayo bonyeza alama ya kusikiliza masikioni hapo chini.

Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri :Mohammed AbdulRahman.