1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi bado haijathibitisha sababu za kifo cha Navalny

19 Februari 2024

Wachunguzi wa Urusi bado hawajathibitisha sababu za kifo cha kiongozi wa upinzani, Alexei Navalny, na haijulikani ni muda gani watafanya hivyo. Kauli hiyo ameambiwa mama wa Navalny.

https://p.dw.com/p/4cYyt
Waombolezaji wa kifo cha Navalny
Waombolezaji waliojitokeza mtaani kupaza sauti kuhusu kile walichokitaja utata wa kifo cha Navalny,Picha: ANNEGRET HILSE/REUTERS

 Kwa mujibu wa msemaji wa mkosoaji huyo aliyefariki siku ya Ijumaa mama yake Navalny, Bi Lyudmila, na mawakili wake hawakuruhusiwa leo hii kuingia katika chumba cha kuhifadhia maiti katika jela hiyo. 

Mjane wa Alexei Navalny, Yulia Navalnaya, atafanya ziara mjini Brussels hii leo ambako atakutana na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pamoja na Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel.

Soma pia:Nchi za Magharibi washutumu Urusi kufuatia kifo cha Navalny

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, amesema mwaliko wa Navalnaya unatuma ujumbe mzito wa uungaji mkono kwa wapigania uhuru nchini Urusi na unatoa heshima kwa sifa aliyoiacha Navalny.