1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Qatar huenda zikapokonywa vibali vya Kombe la Dunia

8 Juni 2015

Mkuu wa kamati ya uhasibu wa shirikisho hilo Domenico Scala amesema huenda Urusi na Qatar zikapoteza nafasi za kuyaandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022

https://p.dw.com/p/1Fdcq
Domenico Scala FIFA Co-Interims-Chef
Picha: picture-alliance/epa/E. Leanza

Scala amesema nchi hizo zinaweza kupokonywa vibali ikiwa ushahidi utaonyesha kulikuwa na ufisadi katika shughuli ya kinyanganyiro cha kupata kibali cha kuandaa mashindano hayo. Scala hata hivyo amesema hadi kufikia sasa hawajapokea ushahidi wowote wa kudhihirisha kuwa nchi hizo mbili zilitoa hongo.

Matamshi yake ndiyo ya kwanza kutolewa na afisa wa ngazi ya juu wa FIFA kuwa kuna uwezekano nchi hizo zikapokonywa uenyeji wa mashindano hayo. Maafisa wa idara ya mahakama wa Uswisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu kutolewa kwa kandrasi hiyo ya kuandaa mashindano ya 2018 na 2022 kama sehemu ya uchunguzi wa madai ya ufisadi katika FIFA.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu