1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yajitoa mkataba wa kuzuia usambazaji wa silaha

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CVG3

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametia saini sheria inayoitoa Urusi kutoka mkataba unaozuia usambazaji wa silaha barani Ulaya.Mkataba huo wa mwaka 1999 umeweka kiwango cha idadi ya silaha kubwa zinazoruhusiwa barani Ulaya na hutazamwa kama ni kiini cha usalama katika bara hilo.

Sheria hiyo mpya humaanisha kuwa Urusi haitoziruhusu tena nchi za Shirika la Kujihami la Magharibi-NATO kukagua vituo vyake vya kijeshi. Serikali ya Moscow imesema,hatua hiyo imechukuliwa kupinga mipango ya Marekani ya kutaka kuweka mitambo ya kujikinga dhidi ya makombora nchini Poland na Jamhuri ya Czech.