1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaombwa kufikiria upya uamuzi wake

13 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CazL

WASHINGTON:

Marekani imetoa mwito kwa Urusi kufikiria upya uamuzi wake,baada ya Moscow kujitoa kwenye mkataba muhimu unaozuia usambazaji wa silaha barani Ulaya.Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani,Sean McCormack amesema,uamuzi wa kujitoa kwenye makubaliano hayo ni kosa na utahatarisha udhibiti wa silaha.

Urusi,kuanzia usiku wa manane wa Desemba 12, imejitoa kwenye mkataba huo.Kwa sehemu fulani, hatua hiyo imechochewa na dai la Shirika la Kujihami la Nchi za Magharibi-NATO kuwa Urusi iondoshe majeshi yake kutoka maeneo yaliyojitenga ya Georgia na Moldovia ambayo yalikuwa sehemu ya jamhuri za Soviet Union ya zamani.Urusi pia imehamakishwa na mpango wa Marekani kutaka kuweka mitambo ya kujikinga dhidi ya makombora,nchini Poland na Jamhuri ya Czech.