1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapambana na moto karibu na kituo cha nyuklia

12 Agosti 2010

Urusi imeimarisha jitahada za kuzima moto katika misitu iliyo karibu na kituo cha utafiti wa nyuklia, huku wasiwasi ukizidi kuhusu chembe chembe za nyuklia kutoka misitu iliyochafuliwa wakati wa ajali ya Chernobyl.

https://p.dw.com/p/Ojhi
Fire fighters struggles with a blaze near the village of Kustaryovka, Ryazan region, Russia 10 August 2010. The Russian Emergency Ministry said there were no risk of wildfires erupting at potentially hazardous facilities in Russia. Firefighters in Russia had yet to make significant headway against the worst wildfires in the country's history on Tuesday despite international help, with more than 550 fires still burning, the Interfax news agency reported 10 August 2010. EPA/MAXIM SHIPENKOV +++(c) dpa - Bildfunk+++
Wazima moto wakipambana na moto nchini Urusi.Picha: picture alliance/dpa

Serikali ya Urusi imepeleka treni maalum ya kuzima moto na watu wengine 70 kuwasaidia zaidi ya wazima moto 3,400 wanaopambana na moto kwenye misitu iliyo karibu na kituo kikuu cha utafiti wa nyuklia. Moto haujafika kwenye eneo la kituo hicho cha nyuklia cha Sarov,lakini hifadhi ya misitu iliyo karibu,imeshika moto tangu kiasi ya juma moja lililopita. Kama watu 50,000 wanapambana na moto katika eneo hilo katikati ya Urusi.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya huduma za dharura, Mikhail Turkov, ndege mbili na helikopta mbili zinazunguka eneo la Sarov kuchunguza mkondo wa moto. Amesema, wanajeshi wawili waliuawa walipokuwa wakizuia moto huo kukaribia kituo cha nyuklia cha Sarov. Msemaji wa kituo hicho amelithibitishia shirika la habari la AFP kuwa moto haujafika kwenye kituo hicho na wafanyakazi wake wala hawakuhamishwa, lakini hakutaka kutoa maelezo zaidi.

Hata hivyo kuna wasiwasi mkubwa kuhusu misitu iliyoshika moto ambayo ilichafuliwa na chembe chembe za nyuklia katika mwaka 1986 kufuatia ajali iliyotokea kwenye mtambo wa nyuklia wa Chernobyl.

An aerial view of the Chernobyl nucler power plant, the site of the world's worst nuclear accident, is shown in this May 1986 photo made a few days after the April 26 explosion in Chernobyl, Ukraine. In front of the chimney is the destroyed 4th reactor. Behind the chimney and very close to the 4th reactor is the 3rd reactor which was stopped on Dec. 6, 2000. The final shutdown of the Chernobyl nuclear power plant is scheduled for Dec.15, 2000. (AP Photo) (Bild für Kalenderblatt)
Mtambo wa nyuklia wa Chernobyl ulioripuka katika ajali ya April 26,1986.Picha: AP

Vladimir Stepanov alie mkuu wa kituo kinachoshughulikia masuala ya dharura, anasema, viwango vya miale ya sumu ya nyuklia havikupindukia kiwango cha kawaida. Serikali ya Urusi inajaribu kutuliza hofu kuwa moto huo wa misituni huenda ukatimua chembe chembe za nyuklia zilizoko ardhini. Lakini muasisi wa shirika linalotetea mazingira "Greenpeace" nchini Urusi, Alexei Yablokov anasema, chembe chembe za nyuklia zinaweza kutawanyika umbali wa mamia ya kilomita kwa kutegemea hali ya hewa.

Wataalamu wanasema Urusi inakabiliana na wimbi la joto kali kabisa katika historia yake. Moto huo umeathiri kila sekta ya maisha na inatathminiwa kuwa pato la jumla la ndani huenda likapunguka kwa asilimia moja.

Mwandishi:P.Martin/AFPE

Mhariri:M.Abdul-Rahman