1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urussi na Marekani zalumbana juu ya mpango wa Makombora ya ulinzi

9 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EYuo

WASHINGTON

Marekani hii leo imesema kwamba Urussi inalenga kuwatia uoga washirika wake wa kimkakati barani Ulaya kuhusiana na mpango wake wa makombora ya ulinzi katika eneo la Ulaya mashariki.

Matamshi ya Marekani yametolewa baada ya Urussi hapo jana kutishia kutumia nguvu za kijeshi kupinga hatua yoyote ya kuweka makombora hayo karibu na mipaka yake.Mapema hapo jana waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice alitiliana saini mpango wa mwanzo wa makombora ya ulinzi na jamhuri ya Czech mjini Prague.Makubaliano hayo yanairuhusu Marekani kujenga na kuendesha kambi ya mitambo ya radar karibu na mjini Prague kama sehemu ya mpango kamili wa kuweka makombora ya ulinzi katika eneo hilo.Marekani inadai mpango huo ni muhimu katika kuzuia mashambulio yoyote ya maadui kama vile Iran dhidi ya washirika wake.Mpango huo bado haujakubaliwa na Poland wakati raia wa Jamhuri ya Czech wanaoupinga huku serikali huenda ikabidi itegemee kura za upinzani katika kuuidhinisha mkataba huo kamili.