1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama mbovu waathiri sekta ya utalii Kenya

Josephat Nyiro Charo1 Agosti 2014

Kisiwa cha Lamu kimepata pigo kubwa katika sekta ya utalii kufuatia mauaji ya Mpekletoni na Kindi mwezi Juni mwaka huu 2014

https://p.dw.com/p/1CnPK
Insel Lamu Kenia
Picha: picture-alliance/dpa

Hali ya sekta ya utalii nchini Kenya inazidi kuwa mbaya huku hali ya usalama ikiwa bado haijaimarika hususan katika pwani ya Kenya. Idadi ya watalii wa ndani na wa mataifa ya kigeni wanaoitembelea imepungua kufuatia tahadhari zilizotolewa hivi karibuni na mataifa ya kigeni kuwashauri raia wao wasizuru nchi hiyo kwa sababu za usalama. Utalii katika kisiwa cha Lamu umeathiriwa sana na mashambulizi yaliyodaiwa kufanywa na kundi la al Shabaab huko Mpeketoni na Hindi, ambapo watu kadhaa waliuwawa.

Kampuni ya TPS East African inayomiliki hoteli za Serena, majumba ya kifahari na kambi za watalii, imeikosoa vikali Bodi ya Utalii ya Kenya kwa kutoa takwimu wiki iliyopita ikisema idadi ya wageni wanaoingia Kenya imepungua kwa asilimia 4 tu ikilinganishwa na mwaka uliopita. Kampuni hiyo imesema takwimu za bodi hiyo ni za mzaha kwani utalii Kenya uko taabani. Josephat Charo amezungumza na Clinton Ngonyo, Meneja wa kampuni ya Utalii ya Lamu Holiday Solutions kuhusu tatizo hili. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Khelef