1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama waimarishwa kueekea uchaguzi Zimbabwe

30 Julai 2013

Polisi wakupambana na ghasia waliojihami wamesambazwa kote nchini Zimbabwe ili kuimarisha usalama wakati huu ambapo nchi hiyo inajitayarisha kufanya uchaguzi wake siku ya jumatano 31.07.2013

https://p.dw.com/p/19HMl
A SADC (Southern Africa Development Community) election observer looks on as Zimbabwe security forces queue to vote during the special voting day for registered members of the police and army in Harare on July 14, 2013. Zimbabwe security forces voted on July 14 in an early election marred by delays over a lack of ballot papers just over two weeks before crucial presidential polls. AFP PHOTO / Jekesai Njikizana (Photo credit should read JEKESAI NJIKIZANA/AFP/Getty Images)
Simbabwe Wahlen Juli 2013Picha: Jekesai Njikizana/AFP/Getty Images

Kulingana na televisheni ya kitaifa nchini humo maelfu ya maafisa wamepelekwa katika eneo la katikati mwa mji na mikoani huku magari yaliokuwa yamebeba silaha yakionekana kupiga doria katika miji ya Harare na Mbare.

Maeneo ambayo maafisa polisi walikuwa wanapiga doria ni maeneo yalio na wafuasi wengi wa waziri mkuu Morgan Tsvangirai na ambayo pia yalishuhudia ghasia katika uchaguzi wa 2008 ambako watu 200 wa chama cha MDC cha waziri mkuu waliuwawa.

Uchaguzi wa mwaka huu wa urais pamoja na bunge unanuiwa kumaliza miaka minne ya uongozi wa serikali ya muungano kati ya Rais Robert Mugabe wa chama cha ZANU-PF na Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC.

Waziri mkuu, Morgan Tsvangirai.
Waziri mkuu, Morgan Tsvangirai.Picha: AP

Huku kukiwa hakuonekani hali ya kuaminika ni vigumu sana kueleza iwapo Tsvangirai aliye na umri wa miaka 61 atafanikiwa kweli katika juhudi zake za kumuondoa madarakani rais wa sasa Robert Mugabe aliye na umri wa miaka 89 ambaye ameiongoza nchi hiyo kuanzia ijipatie uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1980.

Uchaguzi kufanyika Jumatano

Hata hivyo waangalizi wa kura wa nchi za Magharibi wamepigwa marufuku ya kufuatilia uchaguzi huo na kazi hiyo kupewa waangalizi 500 wa kanda na wengine 7000 wa ndani ya nchi. Matokeo ya rasmi uchaguzi yanatarajiwa kutolewa baada ya siku tano lakini huenda pia yakajulikanamapema.

"Mugabe ni mmoja wa viongozi wakongwe duniani na tena ni mmoja wa madikteta wanaotawala anajaribu kutumia mbinu nyengine ya kuiba kura kuliko ile iliotumiwa na ZANU-PF katika kampeni zake zilizopita," alisema Morgan Tsvangirai

Siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi chama cha upinzani kimetoa ushahidi kwa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika unaonesha chama tawala kinapanga njama za kuiba kura.

Rais Robert Mugabe.
Rais Robert Mugabe.Picha: AP

Hata hivyo akizungumza na waandishi habari nchini humo Rais Robert Mugabe amesema ataachia ngazi iwapo atashindwa katika uchaguzi. Mugabe ameiongoza Zimbabwe kwa miaka 33.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mahriri: Mohammed Abdul-Rahman