1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Usalama waimarishwa Ujerumani

Kabogo Grace Patricia19 Novemba 2010

Usalama huo umeimarishwa kutokana na kuwepo taarifa za wapiganaji wenye itikadi kali ya Kiislamu kutaka kufanya mashambulio ya kigaidi.

https://p.dw.com/p/QDEX
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere.Picha: dapd

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere ambaye alitoa tahadhari ya mashambulio ya kigaidi siku ya Jumatano, amesema kuwa watu lazima walindwe na mashambulio hayo ambayo huenda yakawa sawa na mauaji ya watu 166 yaliyotokea mjini Mumbai mwaka 2008.

Akizungumza katika televisheni ya umma, De Maiziere alirudia kusema kuwa hata hivyo, watu wa Ujerumani wanatakiwa kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao za kila siku kama kawaida.

Usalama umeimarishwa katika viwanja vya ndege na vituo vya treni kutokana na kuwepo taarifa za kuaminika za kijasusi kwamba wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu wanapanga kufanya mashambulio kabla ya kumalizika kwa mwezi huu wa Novemba.