1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushahidi wa vidio kutumika CHAN 2018

12 Januari 2018

Teknolojia ya msaada wa vidio kwa waamuzi wa kandanda, maarufu kama VAR, utaanza kutumika kwa mara ya kwanza barani Afrika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika CHAN yatakayofanyika Morocco.

https://p.dw.com/p/2qjtp
Teknolojia ya kutathmini magoli
Picha: picture-alliance/dpa

Mfumo  huo unaruhusu  maafisa  walioko  nje  ya  uwanja  kusaidia  waamuzi  katika  mchezo  katika  masuala  kama  linalooingia  goli, mikwaju  ya  penalti, kadi  nyekundu  na  inapotokea  mchezaji  ameadhibiwa  kwa  makosa. 

Mfumo  huo  umetumika  katika  ligi  ya  Italia Serie A na  Bundesliga nchini  Ujerumani msimu na  unaanza  kutumika  kwa  mara  ya  kwanza  pia  katika  ligi  ya  Uingereza  wiki  hii. 

Teknolojia  hiyo inatarajiwa  kuanza  kutumika  nchini  Morocco  wakati  michezo  hiyo  itakapofikia  robo  fainali , ambapo timu  zinazoshiriki  zinatumia  wachezaji wanaocheza  ligi  za  ndani. Timu  16  zinashiriki. Mashindano hayo  yalitarajiwa  kufanyika  nchini  Kenya lakini nchi  hiyo  ilishindwa kutekeleza  mashariki  ya  shirikisho  la  kandanda barani  Afrika CAF na  Morocco  iliteuliwa kuchukua  nafasi  hiyo.