1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushiirikiano wasaidia Malengo ya Maendeleo ya Milenia

P.Martin14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbWe
UNICEF/ HQ06-0024/Sara Cameron KENYA: Abdi Nasser Mohammed, 10, sits on the parched ground with his one-year-old brother, Imram, in an area on the outskirts of Garissa Town in North Eastern Province. He is looking after the younger child while their mother searches for food in the town. Some 200 families displaced by the drought - mainly children, women and elders - are sheltering in this area. More families arrive each day. Most have lost all of their livestock in the drought and have little meansof support.
UNICEF:Badala ya kwenda shule mtoto mkubwa humtazama mdogo wake wakati mzazi akitafuta chakula .Picha: UNICEF

Kwa mujibu wa Shirika la Watoto Duniani la Umoja wa Mataifa-UNICEF,ushirikiano ulioimarika kati ya nchi zinazoendelea unanufaisha maisha ya watoto masikini kote duniani.Ushirikiano wa aina hiyo hasa unasaidia katika miezi muhimu ya mwanzo ya maisha ya watoto hao.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na UNICEF na kuitwa „Maendeleo kwa Watoto“ imeeleza sehemu gani zilizofanikiwa kufanya maendeleo.Wakati huo huo imesisitita umuhimu wa kuchukuliwa hatua zaidi za dharura.Katika matayarisho ya ripoti hiyo,nchi nyingi zimezingatiwa na habari zilizokusanywa ni za hivi karibuni hasa za mwaka 2006.Huo ni takriban nusu ya muda uliopangwa kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.

Kwani katika mwaka 2000,madola ya kimataifa na taasisi kuu za maendeleo,ziliweka malengo manane. Miongoni mwa malengo hayo ni kupunguza kwa nusu umasikini na njaa kote duniani:watoto wawe na haki ya kupata elimu ya msingi:kupunguza vifo vya watoto na vya mama watoto:kupiga vita UKIMWI, malaria na magonjwa mengine:pamoja na kuhifadhi mazingira na kuendeleza ushirikiano kati ya madola ya Kaskazini na Kusini ili kuleta maendeleo. Azma ni kutimiza malengo hayo,ifikapo mwaka 2015.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon amesisitiza umuhimu wa kuwepo ushirikiano kati ya kambi ya Kaskazini na Kusini ili malengo hayo yaweze kutekelezwa katika kipindi cha miaka minane ijayo.

Maendeleo makubwa yaliyosisitizwa katika ripoti ya UNICEF ni kupunguka kwa vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.Kwa mara ya kwanza katika historia ya sasa,kote duniani idadi ya vifo vya watoto wa umri huo,imepunguka hadi milioni 9.7.Hilo ni punguzo la asilimia 60 kulinganishwa na takwimu za mwaka 1960.

Hata idadi ya watoto wanaokosa elimu ya msingi imepunguka.Kwa mfano kati ya mwaka 2005 na 2006 ni watoto milioni 91 waliokosa elimu ya msingi kulinganishwa na milioni 115 katika mwaka 2002.

Na kuhusu UKIMWI,kuna ushahidi kuwa maendeleo yamepatikana katika baadhi ya nchi za Kiafrika. Mojawapo ni Ethiopia ambako serikali imeanzisha mradi mkubwa wa kuwafunza wafanyakazi 30,000 kutoa huduma za afya katika jamii.

Nchi nyingi, kusini mwa Afrika zimevutiwa na mradi huo kama njia mojawapo ya kukwepa kizingiti kikuu katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia yaani uhaba wa pesa katika mifumo ya afya na tatizo la kutofahamu vizuri njia za kujikinga dhidi ya virusi vya UKIMWI.Takriban theluthi mbili ya watu wote walio na virusi vya HIV na UKIMWI,huishi kusini mwa Sahara barani Afrika.